Ijumaa, 20 Machi 2015

Hii ndio kauli ya Tanesco kutokana na umeme kukatika mara kwa mara

Shirika la umeme nchni- Tanesco - limesema
hakuna mgao wa umeme na kilichojitokeza
kufuatia kukatika kwa umeme mara kwa mara
kuanzia machi 15 ni uchakavu wa
miundombinu ya umeme ikiwemo kuanguka
kwa nguzo za umeme hususani katika maeneo
ya makazi ya watu yasiyopimwa .
Akizungumza na waandishi wa habari, baada
ya baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam
na vitongoji vyake kukosa umeme kwa wakati
tofauti kuanzania machi 15 hadi 18 mwaka
huu, meneja wa kanda wa Tanesco , mhandishi
Mahenge Mugaya amesema changamoto kubwa
inayoikabili Tanesco ni uchakavu wa nguzo na
nyaya za kusafirisha umeme ambapo katika
baadhi ya maeneo yasiyopimwa kumekuwa na
tatizo la magari kugonga nguzo na umeme
hali inayosababisha mitambo ya shirika hilo
kukata umeme ili kuzuia madhara kwa jamii .
Aidha amesema shirika la umeme nchni
limetenga bajeti ya shilingi bilioni 10 katika
mpango wa miaka mitatu wa kuimarisha
umeme katika jiji la Dar es Salaam , mpango
utakaowezesha kuondoa nguzo mbovu , miti
iliyokatika njia za umeme na kuimarisha
vituo vidogo vya kusambaza umeme na
kusisitiza shirika hilo limeshafanya tathimini
ya nguzo mbaovu zote katika njia za umeme
na kuandaa mpango kazi ili kuwa na mfumo
mzuri wa usambazaji umeme .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni