Jumamosi, 28 Machi 2015

Abdu bonge afariki Dunia

Boss was kundi la muziki la tip top connection Abdu bonge amefariki dunia usiku huu huku chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana swahilivibetz inatoa pole kwa wanafanilia na wanatiptop tutakujulisha kwa kila litakalo tufikia

Mawaziri wanne waachishwa kazi kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewasimamisha kazi kwa mda mawaziri wake wanne pamoja na maafisa wengine 12 wa ngazi ya juu katika serikali yake kufuatia madai ya ufisadi.

Waziri mwengine wa tano amejiondoa afisini akisubiri kuchunguzwa na madai hayo.

Maafisa hao walitajwa katika ripoti ya ufisadi mapema wiki hii na tume ya ufisadi nchini Kenya .

Kashfa hizo za ufisadi zinadaiwa kuzikabili wizara za Uchukuzi,Kawi,Kazi na kilimo.

Rais Kenyatta ameipa tume ya kukabiliana na ufisadi siku 60 kuchunguza madai hayo.

Ijumaa, 27 Machi 2015

Funza zaidi ya 100 wagundulika puani mwa mtu

Mwanamume mmoja amekutwa na kuondolewa funza wapatao mia moja walio hai tena wanao kula kula puani mwake na kuruhusiwa aende nyumbani .Mwanamume huyo anatajwa kuwa na umri wa miaka sitini na mitano ,na watabibu wanasema funza hao walikuwa wamejichimbia ndani zaidi ya pua yake.

Mwanamume huyo ni mwenye asili ya Sao Paulo, nchini Brazil,alikuwa akisumbuliwa mno na njia ya mfumo wa hewa hasa puani ,na pua yake ilikuwa imeathiriwa na mabuu ya inzi.

Pamoja na mambo mengine, mara kwa mara mwanaume huyo alikuwa akilalamika kuwa kuna minyoo pia huwa inadondoka kutoka puani mwake.

Tundu za pua ni mahali ambapo vijidudu virukavyo huweza kutaga mayai yao hapo na baadaye hugeuka kuwa funza.

Na wataalamu wa pua na koo wanasema kwamba chakula kikuu cha funza wakaao puani ni nyama za pua na endapo mgonjwa ataachwa bila kupatiwa matibabu ,funza hao wanauwezo wa kutafuna na kuharibu kabisa mfupa wa mwanzi wa pua,kuharibu vimishipa vya uso,pua na macho.

Na hali hiyo ikitokea,jua kutakuwa na maambukizi kwenye ubongo na macho na kwa kawaida husababisha ugonjwa wa uti wa mgongo na hata kifo.

Mwanaume huyo aliamua kwenda kwenye zahanati nchini Brazil kutoa malalamiko yake kwamba siku mbili nyuma aliona kitu kinachofanana na mnyoo ukichomoza na hatimaye kutoka katika pua yake upande wa kushoto.

Funza wakiwa puani

Mwanaume huyo anaishi na virusi vya ukimwi ana tatizo la ini,na kinga yake ya mwili ilikuwa inapungua kwa kasi kubwa na alikuwa hajaanza kutumia vidonge vya kurefusha maisha.

Miaka mitano iliyopita alifanyiwa upasuaji wa pua yake baada ya kugundulika kuwa alikuwa na uvimbe puani na hakuona dalili yoyote hapo kabla,ingawa kwa wiki nzima kabla ya kuhudhuria zahanati alikuwa akitokwa na damu puani,maumivu ya pua upande wa kushoto

Na harufu mbaya,alikuwa akishindwa kupumua sawa sawa na uvimbe ulianza kuonekana usoni na puani mwake.

Lakini baada ya kudumbukiza kijikamera kidogo puani mwake ,aligundulika

Madaktari wakaanza kuwatoa funza hao kwa muongozo wa kamera iliyokuwa ikiangaza puani na kuitibu pua yake.

Iliwachukua siku nne madaktari kuondoa uambukizo katika pua ya mwanaume huyo na baada ya hapo madhila yake yakakoma na baada ya uangalizi wa mwisho kwa kutumia kamera ile ile imethibitika kwamba tatizo lake lime kwisha.

Brazil yaipiga ufaransa 3-1

Timu ya Taifa ya Brazil

Brazili jana aliikimbiza mchamchaka Ufaransa baada ya kuichabanga magoli matatu kwa moja.

Haikuwasaidia Ufaransa kuanza kuona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli lililofungwa na Raphael Varane kwani ni kama waliichokoza kundi la nyuki kwani goli hilo lilirudishwa na Oscar dos Santos Emboaba Júnior katika dakika ya 40, na hatimaye kushindiliwa magoli mengine mawili kupitia kwa Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi hiyo inamalizika Brazil 3 Ufaransa 1.

Katika mechi nyingine za kimataifa za kirafiki zilizochezwa hapo jana, Bahrain iligeuzuwa chapati na Colombia pale waliposhindiliwa magoli 6 kwa mtungi huku Iran ikiwapa darasa Chile kwa kuichabanga magoli mawili kwa nunge.

Leo kutakuwa na mechi moja ya kimataifa ya kirafiki ambapo Canada watairibisha Guatemala

Jumatano, 25 Machi 2015

Timu ya kriketi ya Tanzania kuchuana na Uganda

Tanzania imepangwa kucheza na Uganda katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya Afrika Ligi Daraja la 1 itakayofanyika nchini Afrika ya Kusini katika mji wa Benoni mwishoni mwa wiki hii.

Chama cha Kriketi nchini Tanzania kimeteua timu ya taifa kwa ajili ya michuano hiyo na tayari timu hiyo imeondoka Tanzania kuelekea Afrika ya Kusini.

Nahodha wa Tanzania, Hamisi Abdallah amesema Uganda sio timu ngeni na wanaichukulia mechi yao kwa umuhimu mkubwa.Nchi nyingine zinazotegemewa kushiriki michuano hiyo ni Kenya, Namibia, Botswana na Ghana.

Abdallah anaendelea kuwa nahodha wa timu hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja (miaka 10) akiwa na uzoefu wa kutosha wa michuano ya kimataifa, huku akiwa na rekodi ya kucheza kriketi nchini Uingereza katika klabu ya Watford Town.

Wachezaji wengine waliochaguliwa katika timu hiyo ni Abhik Patwa, akiwa na rekodi ya kufunga nusu century ( runs 50) katika michuano iliyopita ambapo Nigeria na Ghana waliibuka vinara.

Wachezaji wengine ni Yakesh Patel, Ally Mpeka, Arshan Jassani, Riziki Kiseto, Zamoyoni Jabeneke,Harsheed Chohan, Issa Kikasi,Kassim Nassoro, Arun Dagar, Khalil Rehemtullah,Martin Mwarabu na Rahil Amarshi,

Angelina jolie akatwa nyumba ya uzazi

Muigizaji Angelina Jolie amelazimika kutoa mishipa ya kupitisha mayai na vifuko vya mayai baada ya uchunguzi kuonesha kuwa alikuwa katika hatari ya kuathirika na saratani ya nyumba ya uzazi.

Muigizaji huyo maarufu wa Hollywood ameidokezea jarida la New York Times, kuwa alilazimika kutoa uzazi wake juma lililopita katika upasuaji wa dharura.

''Upasuaji huo ulitokana na ripoti ya uchunguzi wa daktari uliobaini kuwa nilikuwa na asilimia 50 ya chembechembe zenye hatari ya kuambukizwa saratani'' alisema Bi Jolie

Habari hizi zimewashtua wafuasi na mashabiki wa totoshoo huyo ambaye miaka miwli tuy iliyopita alilazimika kukatwa matiti kwa sababu ya tishio hilohilo la Saratani.

Aidha mamake muigizaji huyo nyota aliaga dunia kufuatia hitilafu iliyotokana na matibabu ya saratani.

''Sio jambo rahisi sana kukabiliana na swala hili gumu linalohusu afya yangu'' alisema Jolie.

Jolie ambaye ni mkewe muigizaji nyota wa Holywood ctor Brad Pitt, anasema kuwa vipimo vilionesha chembechembe za maradhi hayo na ikamlazimu kuchukua hatua hiyo mara moja.

Wawili hao wanawatoto sita.

Mamake tayari aliaga dunia kutokana na Saratani

''Nilimpigia simu akiwa Ufaransa na akarejea nyumbani mara moja ,lakini cha msingi ni kuwa ukikabiliwa na masaibu kama haya ya kiafya na uwe una mtu anayeweza kukusaidia kwa kukuchangia mawazo mzigo unakuwa mwepesi zaidi''

''Mamangu aligunduliwa kuwa na saratani akiwa na umri wa miaka 49 hivi sasa nina miaka 39 ''

''Licha ya hayo hivi sasa nimeshakoma kuzaa kwa hivyo ninatarajia mabadiliko mengi katika mwili wangu .Hivi sasa sina hamu ya kupata watoto wengine ,alisema jolie.

“Nitastahimili kwa njia ileile ambayo nafikiri maelfu ya wanawake wamepitia''

''Nilijiambia mwenyewe ni lazima nijikaze na kuwa na nguvu maanake sikuwa na sababu ya kujifikiria mimi bila kuona watoto wangu wakijuta na kusema looo! mamangu alikufa kutokana na saratani ya nyumba ya uzazi'' alisema bi Jolie.

Jumanne, 24 Machi 2015

Breaking News:Ajali nyengine ya ndege Ufaransa

Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 imeanguka katika milima ya Alps nchini ufaransa.
Ndege hiyo ulikua imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitokea Barcelona Hispania kuelekea Duesseldorf
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la la Ujerumani Lufthasa chini ya nembo ya Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne

Haya ndio madhara ya mvua zinazoendelea kunyesha Dar

na nguzo ya umeme na kuwaunguza. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi wa Temeke, Zakaria Sebastian alisema vifo vya watu hao watatu vilitokea katika eneo la Mchikichini Kimbangulile, Mbagala. Sebastian aliwataja waliokufa kuwa ni Ramadhan Said (10), mwanafunzi wa darasa la nne Shule ya Msingi Mchikichini, Alhaji Jumanne (15), mwanafunzi wa kidato cha kwanza Shule ya Sekondari ya Charambe na Monica Elistone (26). Alisema wakati mvua ikiendelea kunyesha, watu hao walijihifadhi kwenye kibanda kilichotengenezwa kwa mabati na ghafla waya wa nguzo hiyo ulikatika na kuangukia kibanda hicho na kushika moto. “Wakiwa kwenye banda hilo, ghafla nguzo ilianguka na waya wake kuangukia kibanda kilichoshika moto na kuwateketeza watu hao,” Sebastian. Mjumbe wa shina namba nne wa mtaa huo, Kondo Namna alisema zaidi ya  nguzo saba zimeinamia kwenye nyumba za watu na wameshatoa taarifa Tanesco, lakini hadi jana, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na shirika hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema wakati mvua zinaendelea kunyesha saa sita usiku wa kuamkia jana, mkazi wa Mwananyamala Edward Warioba (22) alifariki dunia baada ya kuangukiwa na ukuta akiwa amelala nyumbani kwake. Katika tukio jingine, Kamanda Wambura alisema maiti ya mwanamume mwenye umri wa kati ya miaka 45 na 50 iliokotwa ikielea kwenye makutano ya Mto Goba na Makongo. Alisema huenda mtu huyo alisombwa na maji ya mvua katika eneo ambalo bado halijajulikana. Wakati maafa hayo yakitokea, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),imetoa tahadhari ya kuwapo kwa mvua kubwa katika maeneo ya ukanda wa Pwani na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuwa makini.

Huu ndio utajiri wa Babu wa Loliondo

Yule babu wa samunge Ambikile Masapila alie kua akitibu watu kwa kikombe apata utajiri wa ajabu hebu jionee mwenyewe kwenye hizi picha

Dunia yaomboleza kifo cha Lee Kuan Yew

Waziri mkuu mwanzilishi wa Singapore, Lee Kuan Yew amefariki dunia.

Lee amefariki akiwa na umri wa miaka tisini na mmoja kutokana na ugonjwa wa mapafu.

Kwa miongo mitatu ya utawala wa Lee alifanikiwa kuipitisha nchi yake katika kipindi cha mpito na kuleta mabadiliko makubwa

ya kiuchumi hasa katika usafirishaji majini kwa kutumia rasilimali kidogo walizokuwa nazo na sasa kuwa kitovu kikubwa cha kibiashara cha kimataifa.

David Adelman ni balozi wa zamani wa Marekani nchini humo, ametuma salamu zake za rambi rambi.

Kifo cha Lee ni mwisho wa enzi zake.

mwisho wa mwanamume mwenye nguvu ya ushawishi aliyeingia madarakani katikati ya miaka ya sitini .

Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani ambao umedumu hata leo

Waombolezaji wakiweka mashada ya maua mbele ya hospitali aliyofia baba Lee Kuan Yew.

na unaweza kuvuka mipaka sio kwa singapore tu bali hata kwa watu wa Asia ya kusini Mashariki.

Viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kutuma risala za rambirambi kwa Singapore, baada ya kifo cha Lee Kuan Yew hospitalini.

Yew aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua homa ya mapafu.

Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia.

Marehemu Lee ambaye aliiletea mabadiliko makubwa taifa la Singapore na kuwa na mojawepo ya bandari maarufu zaidi Duniani huku uchumi wa nchi hiyo ukiimarika maradufu, atasalia katika kumbukumbu la taifa hilo.

Mwanawe ambaye ni waziri mkuu wa sasa nchini humo, Lee Hsien Loong, anasema kuwa Singapore haitawahi kuwa na mtu kama huyo tena.

Lee alifanikiwa kuanzisha ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi yake na Marekani

Katika risala zake za rambirambi, Rais Barrack Obama wa Marekani amemtaja kama gwiji wa historia.

Nchini Uchina, wizara ya mashauri ya nchi za kigeni imemsifia na kumtaja Lee Kuan Yew, kama kiongozi wa kipekee wa bara Asia.

Naye waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, anasema kuwa Bwana Lee alikuwa mmojawepo wa viongozi wakuu duniani.

Serikali ya Singapore imetangaza siku sita ya maombolezo, hadi atakapozikwa siku ya Jumapili.

Wanasoka wanje kupunguzwa england

Baadhi ya wachezaji wa kiafrika watakaathirika na sheria hiyo.

Shirikisho la kanda kanda nchini England FA sasa linakusudia kuandaa sheria itakayo kupunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya watakaosajiliwa katika ligi za nchi hiyo.

Mwenyekiti wa shirikisho hilo Greg Dyke asema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye hatari ya kutowasaidia wachezaji raia wa Uingereza kama hatua hazitachukuliwa.

Katika mpango pia itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji waliokulia nchini humo.

Mikakati hiyo yote ni ya kuimarisha timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za kimataifa.

Jumatatu, 23 Machi 2015

Safari za ndege za Kenya Airways zarejeshwa

Hatimaye marais Uhuru Kenyetta wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania wamekubaliana kufutilia mbali maagizo ya Mamlaka ya anga nchini Tanzania kupunguza idadi ya ndege za Kenya zinazotua nchini Tanzania na agizo la Wizara ya maliasili ya Kenya kupiga marufuku magari ya Tanzania kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Katika makubaliano hayo ndege za Kenya Airways sasa zitafanya safari zake kama kawaida nchini Tanzania na magari ya Tanzania yataruhusiwa kuchukua watalii na abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernald Membe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya viongozi hao wakuu wa nchi hizo mbili kukutana nchini Namibia walikokwenda kuhudhuria maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia na kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo.

Awali kabla ya uamuzi wa marais hao, magari ya Tanzania yaliyokuwa yakichukua watalii katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, yalipigwa marufuku na serikali ya kenya katika agizo lililotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii Phyllis Kandie, ambapo baadae Tanzania nayo kupitia mamlaka ya Anga ya nchi hiyo ikaagiza ndege za shirika la ndege la Kenya, Kenya airways zinazoingia Tanzania kupunguza safari kutoka 42 kwa wiki hadi 14 pekee.

Makubaliano ya marais hao yanakuja siku chache baada ya mzungumzo ya mawaziri wa utalii wa Tanzania na Kenya kuvunjika mwishoni mwa wiki kufuatia pande hizo mbili kushindwa kufikia muafaka kuhusu magari ya Tanzania yaliyopigwa marufuku uwanja wa Jomo Kenyatta. Huku pia mamlaka ya anga ya Tanzania na ile ya Kenya nazo zikishindwa kufikia muafaka kuhusu kupunguza safari za ndege za kenya zinazoingia Tanzania

Jumamosi, 21 Machi 2015

Zito kabwe ahamia rasmi ACT

Hayawi hayawiSasa yamekuwa! Licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya jana Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.

Hii inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani yachama hicho.


Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi 
waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari 
Jumapili ya Machi 22. 

NB: ACT-Tanzania: kirefu chake ni : Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.


Mwanachama rasmi wa ACT, Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.


“He..he he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi hiyo 
kwa baadhi ya wanachama waliosimama (hawapo pichani) nje ya ofisi za chama cha ACT,
tawi la Tegeta.


Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya 
kupokea kadi hiyo.


Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.


Mh. Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama
hicho mapema leo.


Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa leo.

Ijumaa, 20 Machi 2015

Kenya airways yapunguza safari zake Dar

AirwaysShirika la ndege la Kenya, Kenya Airways
leo limeanza rasmi kupunguza safiri zake katika
uwanja wa ndege wa Dar es Salaam kufuatia agizo
la mamlaka ya anga ya Tanzania kuamuru shirika
hilo kupunguza safari zake kutoka 42 kwa wiki
hadi 14.
Kenya Airways
Serikali ya Tanzania inasema huo ndio
mkataba wa tangu awali na kulaumu mamlaka
ya anga nchini Kenya kwa kushindwa kuafikia
maelewano na mamlaka ya Tanzania kuhusu
jambo hilo.
Tayari baadhi ya wasafiri wanaotumia ndege
za shirika hilo wameanza kuathirika kufuatia
shirika hilo kufuta baadhi ya safari kutoka
Dar es Salaam

Hii ndio kauli ya Tanesco kutokana na umeme kukatika mara kwa mara

Shirika la umeme nchni- Tanesco - limesema
hakuna mgao wa umeme na kilichojitokeza
kufuatia kukatika kwa umeme mara kwa mara
kuanzia machi 15 ni uchakavu wa
miundombinu ya umeme ikiwemo kuanguka
kwa nguzo za umeme hususani katika maeneo
ya makazi ya watu yasiyopimwa .
Akizungumza na waandishi wa habari, baada
ya baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam
na vitongoji vyake kukosa umeme kwa wakati
tofauti kuanzania machi 15 hadi 18 mwaka
huu, meneja wa kanda wa Tanesco , mhandishi
Mahenge Mugaya amesema changamoto kubwa
inayoikabili Tanesco ni uchakavu wa nguzo na
nyaya za kusafirisha umeme ambapo katika
baadhi ya maeneo yasiyopimwa kumekuwa na
tatizo la magari kugonga nguzo na umeme
hali inayosababisha mitambo ya shirika hilo
kukata umeme ili kuzuia madhara kwa jamii .
Aidha amesema shirika la umeme nchni
limetenga bajeti ya shilingi bilioni 10 katika
mpango wa miaka mitatu wa kuimarisha
umeme katika jiji la Dar es Salaam , mpango
utakaowezesha kuondoa nguzo mbovu , miti
iliyokatika njia za umeme na kuimarisha
vituo vidogo vya kusambaza umeme na
kusisitiza shirika hilo limeshafanya tathimini
ya nguzo mbaovu zote katika njia za umeme
na kuandaa mpango kazi ili kuwa na mfumo
mzuri wa usambazaji umeme .

Alhamisi, 19 Machi 2015

Mancity kumtema yaya toure


Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City
watamuuza Yaya Toure msimu huu katika mpango
unaolenga kuwauza wachezaji wengine wa kilabu
hiyo kwa lengo la kununua wachezaji chipukizi
watakaoongozwa na mchezaji Kevin De Bruyn wa
Wolfsburg.
Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona
katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya
kombe la vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha
kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika
katika kilabu hiyo.
Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa
katika mechi dhidi ya Barcelona ni Sergio
Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini
ya umri wa miaka 27.
Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet
Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa
na maisha marefu katika kilabu hiyo
,waliosalia huenda wakauzwa.
Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary
Sagna,Martin Demichelis,Alkesandar Kolarov
,Samir Nasri na James Milner ambaye
kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani.
Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa
katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumatano
usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus
Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin
Dzeko huenda pia wakauzwa.
Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili
kujiunga na kilabu ya New York City nchini
Marekani.

Shilole ahamasisha vijana kujiandikisha na Bvr

Kampeni kubwa ya ZamuYako2015 yenye lengo
la kuhamashisha vijana kushiriki katika zoezi
kujiandikisha kupiga kura, imeendelea kupamba
moto ikiendelea kuungwa mkono na wasanii
mbalimbali.
Safari hii mwanadada Shilole akiongea na
vijana hususani wale kutoka Tabora
kuwahamasisha kuwa wao ndio nguvu kazi ya
taifa na wanapaswa kupiga kura.

Sserunkuma avunja mkataba simba

Mbali na hilo, pia uongozi wa Simba
unaendelea kufanya mabadiliko katika nafasi
mbalimbali za viongozi na juzi Jumanne
ulitangaza kumtoa Humphrey Nyasio katika
nafasi ya Ofisa Habari na badala yake
amechukuliwa na Haji Manara, huku ikielezwa
kuwa wapo mbioni kumbadili Katibu Mkuu
wake, Stephen Ally dhidi ya Hamis Kisiwa.

Jumatano, 18 Machi 2015

Kanye west amuanika mkewe mtandaoni

Mshirikishe mwenzako
Mkewe Kanye West Kim Kardashian ambaye
picha zake za utupu ziliwekwa katika
mtandao wa Twitter
Msanii wa muziki Kanye West ameweka msururu
wa picha za utupu wa mkewe Kim Kardashian
West katika mtandao wake wa Twitter.
Nyota huyo wa muziki wa rap aliwagawia
picha hizo takriban watu millioni
11.7,wanaomfuata katika mtandao wa twitter
pamoja na ulimwengu mzima.
Picha hizo zinamuonyesha mkewe Kim
kardhashian akijiziba uchi wake na mikono.
Katika ujumbe wake msanii huyo aliyeimbia
wimbo kwa jina ''Yeezus'' alijigamba kuhusu
hatua zilizopigwa na mkewe katika Runinga
ya Reality TV na kusema ana bahati kuwa
naye.
Kim Kardashian
Katika ujumbe mmoja ambao uliwekwa na picha
ya uchi ya Kardashian akijiziba kifua chake
na mikono,Kanye West aliandika ''NINA
BAHATI''.
Ujumbe huo ulifuatiwa na mwengine pamoja na
picha ya Kim ukimpongeza Kardashian kwa
kupata watu millioni 30 katika mtandao wake
wa kijamii.

Chama cha Likud chashinda uchaguzi Israel

Chama cha Likud cha Waziri Mkuu Benjamin
Netanyahu kimepata ushindi wa kushangaza katika
uchaguzi mkuu wa Israel. Vimeripoti vyombo vya
habari vya Israel.
Matokeo ya awali yalionyesha chama cha
mrengo wa kushoto cha Zionist Union kupata
mshitiko.
Huku kura nyingi zikiwa zimehesabiwa, Likud
kinaonekana kupata viti 29 katika bunge lenye
viti 120, huku chama cha Zionist Union
kikiwa na viti 24.
Matokeo haya yakithibitishwa, itaonyesha
kuwepo kwa serikali nyingine ya mseto
itakayoongozwa na Bwana Netanyahu.
Yitzhak Herzog kiongozi wa chama cha
mrengo wa kushoto cha Zionist Union
Bwana Netanyahu atahitaji kuungwa mkono
kutoka vyama vingine ili kuunda serikali ya
mseto.
Katika hotuba kwa wafuasi wake mjini Tel
Aviv baada ya kufungwa kwa vituo vya
kupigia kura Jumanne, Bwana Netanyahu
amesema tayari amezungumza na viongozi wa
vyama vingine vyenye mrengo wa kulia kuhusu
kuunda serikali mpya "bila kuchelewa".
Bwana Netanyahu amehodhi siasa za Israel
kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka 20.
Kiongozi wa muungano wa vyama vya mrengo
wa kushoto wa Zionist Union Yitzhak Herzog
amekishutumu chama tawala cha Likud kwa
kudidimiza viwango vya maisha ya raia wa
Israel na amekuwa akipiga kampeni dhidi ya
sera za nje za Bwana Netanyahu.

Jumanne, 17 Machi 2015

Arsenal yalala kwa monaco yashindwa kusonga ulaya

Pamoja na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
wakiwa ugenini katika mchezo uliopigwa usiku wa
kuamkia leo, washika bunduki wa jiji la London
Arsenal wameshindwa kusonga mbele katika hatua
ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa
barani Ulaya kwa kosa la kuruhusu magoli mengi
wakiwa nyumbani katika mchezo wa awali,
ambapo Monaco iliwabamiza wenyeji wao hao
Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1.
Arsenal ilijipatia goli la kwanza dakika ya 36
ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Olivier
Giroud kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la
pili katika dakika ya 79 ya mchezo huo.
Matokeo ya jumla kwa timu hizo ni 3-3 japo
Monaco inasonga mbele kwa faida ya kuwa na
magoli mengi ya ugenini na kuwaacha vijana
wa mzee Wenga wakikosa kufika robo fainali
kwa mara ya tano mfululizo. Kitimtimu hicho
cha klabu bingwa Ulaya kilitimua vumbi pia
huko nchini Hispania pale, Atletico Madrid
ilipowakaribisha Bayer Leverkusen kutoka
Ujerumani. Katika mchezo huo wenyeji
Atletico wamefanikiwa kusonga mbele kwa
mikwaju ya Penati baada kumaliza dakika 120
wakiwa mbele kwa bao moja ambalo
halikutosha kuamua mshindi kutokana na
matokeo ya mchezo wa awali ambapo
Leverkusen iliibanjua Atletico bao moja kwa
bila. Wakiwa mbele ya mashabiki wao lukuki
Atletico ilishinda penati 3 dhidi ya 2 za
wageni wao na kutinga moja kwa moja katika
hatua ya robo fainali wakiungana na ndugu
zao Real Madri. Ligi hiyo itaendelea tena leo
hii kwa michezo miwili kupigwa. Borussia
Dortmund watavaana na Juventus huku miamba
ya soka ya Hispania Barcelona ikiialika
Manchester City kutoka England.

Arsenal yalala kwa monaco yashindwa kusonga ulaya

Pamoja na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
wakiwa ugenini katika mchezo uliopigwa usiku wa
kuamkia leo, washika bunduki wa jiji la London
Arsenal wameshindwa kusonga mbele katika hatua
ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa
barani Ulaya kwa kosa la kuruhusu magoli mengi
wakiwa nyumbani katika mchezo wa awali,
ambapo Monaco iliwabamiza wenyeji wao hao
Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1.
Arsenal ilijipatia goli la kwanza dakika ya 36
ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Olivier
Giroud kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la
pili katika dakika ya 79 ya mchezo huo.
Matokeo ya jumla kwa timu hizo ni 3-3 japo
Monaco inasonga mbele kwa faida ya kuwa na
magoli mengi ya ugenini na kuwaacha vijana
wa mzee Wenga wakikosa kufika robo fainali
kwa mara ya tano mfululizo. Kitimtimu hicho
cha klabu bingwa Ulaya kilitimua vumbi pia
huko nchini Hispania pale, Atletico Madrid
ilipowakaribisha Bayer Leverkusen kutoka
Ujerumani. Katika mchezo huo wenyeji
Atletico wamefanikiwa kusonga mbele kwa
mikwaju ya Penati baada kumaliza dakika 120
wakiwa mbele kwa bao moja ambalo
halikutosha kuamua mshindi kutokana na
matokeo ya mchezo wa awali ambapo
Leverkusen iliibanjua Atletico bao moja kwa
bila. Wakiwa mbele ya mashabiki wao lukuki
Atletico ilishinda penati 3 dhidi ya 2 za
wageni wao na kutinga moja kwa moja katika
hatua ya robo fainali wakiungana na ndugu
zao Real Madri. Ligi hiyo itaendelea tena leo
hii kwa michezo miwili kupigwa. Borussia
Dortmund watavaana na Juventus huku miamba
ya soka ya Hispania Barcelona ikiialika
Manchester City kutoka England.

Helikopita ya UN yaanguka mali

Helikopita ya umoja wa mataifa imeanguka
Kaskazini mwa Mali na kuua watu wawili raia
ambao ni wafanyakazi wa ndege hiyo.
Ndege hiyo ni mali ya vikosi vya walinda
amani nchini Mali MINUSMA.Hata hivyo
inadaiwa kuwa UN ina askari wapatao 11,000
kutoka mataifa mbalimbali.
Hata hivyo kwa mjibu wa shirka hilo la umoja
wa mataifa UN,hatua hiyo dhidi ya
wapiganaji hao nchini Mali.Awali mwezi huu
roketi za vikosi vya umona wa mataifa.

Mwanasheria wa daktari wa osama auwawa

Aliyewahi kuwa mwanasheria wa Daktari wa Osama
bin Laden, Samiullah Afridi ameuawa kwa kupigwa
risasi huko Pakistan.
Mtu aliyekuwa na silaha alimmshambulia
Samiullah Afridi ambaye alikuwa ndani ya
gari lake akiendesha eneo la Peshawar.
Samiullah Afridi alikuwa mmoja wa
wanasheria wa Dr.Shakeel Afridi ambaye ndiye
aliyefichua siri kwa Marekani juu ya wapi
alikokuwa Ossama Bin Laden ambaye alikuwa
mafichoni huko Pakistani kwa takribani miaka
minne.
Dr Afridi wakati anauawa alikuwa katima
matembezi alifungwa kifungo cha muda
mrefu.Kundi la Talbani limekiri kutekeleza
mauaji hayo.

Jumatatu, 16 Machi 2015

Kaburi la sadam hussein laharibiwa iraq

Wanajeshi wa Iraq na wapiganaji wanaopigana na wanamgambo wa Islamic State karibu na mji wa Tikrti wanasema kuwa kaburi na la rais wa zamani wa nchi hiyo Saddam Hussein karibu limeharibiwa kabisa.

Picha za shirika la habari za AP zilionyesha mabaki ya kaburi hilo lililojengwa kwa njia ya kifahari lililo katika kijiji cha al-Awja.

Aidha zinaonesha picha za Saddam zikiwa zimeondolewa na mahala pake kuwekwa picha za viongozi wa wapiganaji ikiwemo picha ya jenerali wa Iran Qassem Soleimani anayewashauru wapiganaji wanaopigana vita na islamic state.

Picha zinaoesha kaburi hilo la kifahari likiwa limeharibiwa kabisa

Mwaka uliopita jamii ya wasunni wanaokaa katika eneo hilo liliondoa mwili wa kiongozi huyo wa Iraq ambaye kungolewa kwake madarakani na majeshi ya muungano yaliongozwa na Marekani iliitumbukiza taifa katika vita ambavyo vimechacha hadi leo.

Haijulikani hadi wa leo ulizikwa wapi mwili huo.

Mwandishi wa BBC nchini Iraq anasema kuwa kuna shauku kuwa huenda wapiganaji wa Shia ndio walioharibu kaburi hilo ilikulipiza kisasi cha mateso waliyopita mikononi mwa kundi la Islamic state na wapiganaji wa Sunni.

Breaking news; Ajali ya moto mabibo hostel

Moto mkubwa unawaka maeneo ya hosteli za mabibo wanafunzi wamepoteza vitu vyao vya gharama mpka sasa zimamoto wameshafika na wanamalizia kuuzima moto huo sehemu zilizo athirika zaidi ni ghorofa ya juu chanzo cha moto huo bado hakija fahamika

Jumapili, 15 Machi 2015

Waandishi wa BBC wanaharakati mbaroni Congo DRC

Waandishi wa habari wa kigeni, wanadiplomasia, wanaharakati na wasanii mbalimbali wametiwa mbaroni na polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wakiwemo waandishi wa habari wa BBC.

Wanaharakati hao, ambao ni vijana kutoka nchini Burkina Faso, Senegal na Congo, walikuwa na mkutano na waandishi wa habari kuhusu jukwaa jipya la kijamii.

Mwandishi wa BBC Maud Jullien anaripoti kuwa wanaharakati kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Senegal na Burkina Faso walikuwa na mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kinshasa unaohusu kuundwa kwa jukwaa jipya la kijamii la vijana wa Congo.

Hapo ndipo walipokamatwa na kupelekwa makao ya usalama wa taifa.

Waandishi wa BBC ni miongoni mwa waliokamatwa na wanasema wamewaona polisi wakiwapiga baadhi ya wanaharakati kwa kutumia marungu.

Lambert Mende ambaye ni msemaji wa serikali ya Congo amesema mkutano huo haukuwa halali na kusema kuwa raia waliokamatwa kutoka Senegal na Burkina Faso ni wachochezi hatari kwa usalama wa taifa la Congo.

Nchi ya Burkina Faso na Senegal zote zilikuwa na vuguvugu dhidi ya marais wao walipojaribu kubaki madarakani baada ya muda unaoruhusiwa kwa mujibu wa katiba ya nchi zao kumalizika.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo atakamilisha muhula wake wa mwisho ifikapo Januari, 2016.

Watu zaidi ya arobaini wameuawa katika vurugu zilizosababishwa na muswada wa uchaguzi ambao ungemuongezea muda wa kukaa madarakani.bert MendeCOngo

Jumamosi, 14 Machi 2015

Papa francis atoa ishara za kujiuzulu

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu.

Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya pili tangu achaguliwe,Papa Francis amesema kuwa anahisi kwamba uongozi wake katika kanisa hilo hautaendelea kwa kipindi kirefu.

Amesema kuwa hatua ya Benedict kujiuzulu mwaka 2013 ni ya ujasiri na haifai kuchukuliwa kama ya kipekee.

Papa Benedict ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tangu papa Gregory wa 12 mwaka 1415.

Papa Francis anasema kuwa anatamani maisha yake ya kuwa muhubiri na angependelea kuzuru maeneo kadhaa bila kujulikana.

Ijumaa, 13 Machi 2015

Kesi ya raisi wa kenya yafungwa rasmi

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta .

Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.

Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu.

Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha.

Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.

Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake.

Upandikizaji wa uume wafaulu A.kusini

Kundi la madaktari wa upasuaji kutoka Afrika kusini limefanikiwa upandikizaji wa uume wa mwanadamu.

Oparesheni hiyo iliochukua masaa manane ilifanywa mnamo mwezi Disemba katika hospitali ya Tygerberg mjini Cape Town kupitia ushirikiano wa chuo kikuu cha Stellenbosch.

Inadaiwa kuwa jaribio la pili la upasuaji huo kufanywa.

Madaktari wanasema kuwa mgonjwa aliyefanyiwa upandikishaji huo amepona.

Uume wake ulikatwa baada ya matatizo yaliosababishwa na kupashwa tohara.

Mapokezi ya zito yafunika kigoma awataka wananchi wasimlilie

Baada ya kutemwa na CHADEMA, Zitto Kabwe aenda jimboni kwake Kigoma Kaskazini kuzungumza na wananchi wake. 

LOL na haya ndio mapokezi aliyopata huko jimboni, watu nyomi wamejitokeza kumpokea na kelele zikisikika ..ZITOO...ZITOOO..ZITOOO...


MANENO MENGINE MAGUMU AMBAYO ZITTO AMEWAAMBIA WANA KIGOMA LEO AKIWA KWENYE ZIARA YAKE......

Ikiwa bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa  vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali.

        Akiwa katika ziara yake  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa makini  walishapitia misuko suko kama yake.

       Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya Chama chake na yeye

Zitto ametoa kauli hiyo leo mjini Kigoma alipokutana na viongozi 250 kwenye mkutano wa ndani uliohusisha viongozi  kutoka katika kila kijiji kwenye jimbo la Kigoma kaskazini yenye jumla ya vijiji 45.

Aliwataja baadhi ya  wanasiasa waliopita katika hatua kama yake na baadae wakageuka washindi kuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad(Tanzania),Mahathir Mohamed(Malaysia na Indira Gandhi wa India.

              “Msinililie mimi kwa kuwa haya ni mapito ya kila mwanasiasa Makini,wengi walio makini walitofautiana na vyama vyao kwa sababu ya maslahi ya mataifa yao,wapo walioanzisha vyama baada ya hali hiyo na wakashinda na wapo waliopigiwa magoti na vyama vyao baada ya kugundua walichofanya si sahihi, hivyo jukumu kubwa ni kuniunga Mkono”alisema Zitto.

            Alisema mpaka sasa hajapewa taarifa yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake na kama hali hiyo ikijitokeza atarudi kuwafahamisha juu ya hatua atakayochukua.

             Zitto yupo mjini Kigoma kwa ziara ya siku tatu,ambapo atawatembelea wakulima wa mradi wa Kahawa walio katika mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF), pamoja na kukabidhi gari aina ya Ambulance katika kituo cha Afya Nyarubanda na kisha kufanya mikutano miwili ya hadhara.

       

          Juzi Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu,alitangaza hadharani kuvuliwa uanachama kwa Zitto kutokana na kushindwa katika kesi aliyofungua kupinga asijadiliwe na Chama Chake

Serena akumbushwa alivyodhalilishwa mwaka 2001

Serena Williams

Mcheza tenis mwanadada namba moja kwa ubora duniani Serena Williams amesema haamini kama anaweza kurejea mji Indian Wells huko Calfonia nchini Marekani kushiriki mashindano ya tenis baada ya kudhalilishwa na watazamaji wakati alipokuwa msichana wa miaka 19.

Serena ambaye kwa sasa ana miaka 33 huenda akashiriki tena mashindano ya BNP Paribas Open yatakayofanyika katika mji Califonia baada ya kuyasusia kwa miaka 14.

Alhamisi, 12 Machi 2015

Mikakati ya uchaguzi yaanza Burundi

Chama kinachotawala nchini Burundi kimeanza mchakato wa uteuzi wa mwanachama atakayewania nafasi ya uraisi katika uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Kombe la dunia:zimbabwe lapigwa marufuku

Fifa imepiga marufuku Zimbabwe kwa kushindwa kumlipa kocha wake wa zamani

Zimbabwe imepigwa marufuku kushiriki katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia la mwaka 2018 baada ya kukataa kumlipa kocha wake wa zamani Jose Claudinei Georgini.

Shrikisho la soka FIFA limesema katika taarifa kwamba limechukua hatua hiyo baada ya taifa hilo kushindwa kumlipa kocha huyo.

Fifa imeongezea kuwa shirikisho la soka nchini Zimbabwe ZIFA lilishindwa kulipa deni hilo licha ya kupewa mda wa kufanya hivyo.

Marufuku hiyo inakatiza fursa ya taifa hilo kufuzu katika fainali za kombe hilo nchini Urusi kabla ya kuanza harakati zake za kutaka kufuzu.

Mechi za kufuzu kwa dimba hilo barani Afrika zinatarajiwa kuanza mwezi Octoba huku droo ikifanywa mnamo mwezi Julai mjini St Petersburg.

Zimbabwe haijawahi kufuz