Jumanne, 28 Aprili 2015

Jeshi la Nigeria lawaokoa wasichana 293

Jeshi nchini Nigeria

Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.

Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya kuziharibu kambi hizo.

"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."

Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok.

"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote

Jumamosi, 25 Aprili 2015

Choko choko za wenger na morinho zaanza

Arsene Wenger

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemjibu mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger baada ya Wenger kuhoji kuhusu mbinu inayotumiwa na Chelsea kulinda lango lake.

Wenger alimchokoza kocha huyo wa Chelsea akisema kuwa ni rahisi kulinda lango,swala lililomshinikiza Mourinho kumjibu akisema kuwa iwapo kulinda lango ni rahisi ni kwa nini Arsenal walibanduliwa katika michuano ya kufuzu kwa robo fainali walipolazwa 3-1 na Monaco.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ya ligi ya Uingereza itakayochezwa katika uwanja wa Emirates siku ya jumapili.

Alhamisi, 23 Aprili 2015

Basi laua 10 shinyanga

Habari  zilizotufikia  zinaarifu  kuwa  basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.

Watu 10 wamefariki na  50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.





Jumatano, 22 Aprili 2015

Mama Lulu afunguka mazito kuhusu mwanawe

Kufuatia kuandamwa na skendo za wanaume na kuchafuliwa kila siku, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ ametoa kauli nzito yenye kushtua kwamba anatamani mwanaye huyo afe tu ili watu wanyamaze kumsemasema. Imemuuma sana!

Mama Lulu amefunguka hayo siku kadhaa baada ya mitandao ya kijamii kuchafuka kwa habari za binti yake na wanaume hasa wa watu huku mwenyewe (Lulu) akiwa nyumbani kwake Mbezi-Beach jijini Dar akiwa hana hili wala lile.

Akizungumza na gazeti la Risasi, mama Lulu alisema mambo mazito kuwa, hakuna mzazi ambaye hata siku moja anaweza kuvumilia kuona mtoto wake akiandamwa na kashfa ambazo si za kweli.

“Mimi ndiye nimemzaa Lulu, najua uchungu wa mtoto kama mzazi.
“Wanaomsema Lulu vibaya wakumbuke hata mimi nina moyo kama wao, si chuma hivyo hata mimi naumia kama ambavyo mwanamke yeyote mwenye kujua uchungu wa mwana ni nini anaweza kuumia.“Ni mzazi gani mwenye moyo wa chuma wa kuona mwanaye anabebeshwa shutuma nzito kama hizo kila kukicha halafu akanyamaza au kufurahia?

“Watu wanamfuatilia na kumsakama sana mwanangu. Hawamwachi apumue,” alisema mama Lulu kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

Jumanne, 21 Aprili 2015

Hukumu ya morsi kusomwa leo

Mohamed Morsi

Mahakama nchini Misri inatarajiwa kutoa hukumu kwenye kesi kadha zinazomkabili rais wa zamani Mohammed Morsi ambaye aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013.

Anakabuliwa na kesi pamoja na viangozi wengine wa kundi la Muslim Brotherhood kwa kuwachochea wafuasi kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwaka 2012.

Mawakili wanamtetea bwana Mosri wamasema kuwa huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo. Mamia ya wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood wamehukumiwa kifo katika mikakati ya kukabiliana na kundi hilo lililopiwa marufuku na rais wa sasa Abdul Fattah al-Sisi.

Kundi la Muslim Brotherhood limemlaumu rais kwa kutumia mahakama kama silaha

Ethiopia yaanza cku 3 za maombolezo

Islamic State wakienda kuwaua raia wa Ethiopia

Ethiopia imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na wanamgambo wa kundi la Islamic State nchini Libya.

Bendera zitapepea nusu mlingoti wakati nalo bunge la nchi hiyo likikutana kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya ishirini.

Msemaji wa serikali Redwan Hussein, alisema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani ulaya.

Mungano wa Afrika ambao una makao yake makuu nchini Ethiopia ulilaani mauaji hayo na kusema kuwa utafanya mikakati ya kuhakikisha kuwepo usalama nchini Libya.

Wanamgambo wa Islamic State walitoa kanda ya video ambayo inakisiwa kuonyesha mauaji hayo yanayoonyesha watu hao wakipigwa risasi na kukatwa vichwa.

Jumatatu, 20 Aprili 2015

Wahamiaji 20 zaidi wazama bahari ya mediterania

 Wahamiaji waliokolewa Mediterenian Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo la IOM watu ishirini wameripotiwa kufariki. Aliyetoa ujumbe huo wa dharura amesema, boti tatu zinahitaji misaada katika eneo la kimataifa la bahari hiyo. Mawaziri wa muungano wa Ulaya, EU, wanakutano mjini Luxembourg, leo kujadili mzozo huo wa uhamiaji baada ya mamia ya watu kuzama mwishoni mwa juma lililopita, baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya. Afisa mkuu anayehusika na masuala ya nchi za kigeni wa EU, Federica Mogherini, amesema kuwa mataifa ya bara Ulaya yanapaswa kushughulikia tatizo hilo la wahamiaji katika bahari ya Mediterranean. "Tunawajibika kisiasa na kwa misingi ya kibinadam kutekeleza majukumu yetu. Bahari ya mediterenian ni letu na ni sharti tuchukuE hatua kama raia wa Ulaya. Ni kwa manufaa yetu, hadhi ya muungano wa ulaya na dhamira kuu ya kuundwa kwa muunganoi huu ni kulinda haki za kibinadam, heshima ya binadamu na masiha ya watu, ni lazima tuzingatie hayo'' Alisema Mogherini. Baadhi ya mataifa ya Kusini mwa Ulaya yanasema kuwa hadhi ya EU, imehujumiwa kufuatia uamuzi wake wa mwaka uliopita wa kupunguza shughuli za uokozi. Umoja wa Mataifa umesema njia ya kutoka Kaskazini mwa Afrika hadi Italia na Malta imegeuka na kuwa hatari zaidi duniani.

Zwelithini kutuliza raia south Africa

Goodwill Zwelithini, Mflame wa Zulu

Mfalme wa Jamii wa Wazulu nchini Afrika Kusini, Goodwill Zwelithini, anatarajiwa kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kujiepusha na ghasia, kufuatia kuongezeka kwa mashambulio ya kibaguzi nchini humo.

Mfalme huyo ameshutumiwa kwa kuchochea mashambulio hayo ambayo yamesababisha vifo vya watu saba.

Zwelithini, alinukuliwa akisema kuwa raia wote wa kigeni wanapaswa kurejea katika mataifa yao.

Zaidi ya watu mia tatu wamekamatwa kuhusiana ghasia hizo.

Maelfu ya watu wanatarajiwa kufurika uwanja mmoja ulioko mji wa Mashariki wa Durban kusikiliza hotuba hiyo ya Mfalme Zwelithini.

Amekariri kuwa matamshi yake hayakufahamika.

Miongoni mwa washukiwa waliokamatwa hivi karibuni na wanaume watatu ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya rais mmoja wa Mozambique katika eneo la Alexandra viungani mwa mji mkuu wa Johannesburg.

Picha kadhaa zimeonyesha Emmanuel Sithole akindungwa kisu huku umati mkubwa ukitizama.

Raia moja wa kigeni akishambuliwa nchini Afrika KusiniMama mmoja raia wa kigeni ambaye nyumba yake ilivamiwa nchini Afrika Kusini

Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, amesema mashambulio hayo yanakwenda kinyume na maadili yote wanayoamini.

Makundi kadhaa yaliyojihami yameshambulia na kupora maduka kadhaa yanayomilikiwa na wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika.

Huku idadi ya watu wasio na kazi nchini humo, ikikadiriwa kuwa zaidi ya asilimia Ishirini na nne, raia wengi wa taifa hilo wamewashutumu raia wa kigeni kwa kuchukua nafasi zao za kazi.

Maelfu ya raia hao wa kigeni, wamekimbia makwao na sasa wanaishi katika kambi za muda, ili hali mataifa jirani wameanza shughuli ya kuwahamisha raia wao.

Siku ya Jumapili, serikali ya Zimbabwe imetuma mabasi kadhaa mjini Durban kwenda kuwachukua raia wake wapatao mia nne.

Takwimu rasmi za serikali zinakadiria kuwa kuna raia milioni mbili wa kigeni wanaoishi nchini Afrika Kusini, lakini wengi wanahoji kuwa idadi hiyo huenda ni kubwa zaidi.

Ijumaa, 17 Aprili 2015

Kanye west aanzisha bibilia yake

Kanye West

Hujulikana sana kwa maringo yake,lakini kwa kweli Kanye West asingekufuru na kujitambulisha kama mungu katika biblia hiyo.

Kitabu hicho kitukufu kimebadilishwa na kuwa Biblia ya sasa kwa jina ''Yeezus'' na amini usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho limeondolewa na badala yake msanii huyo wa muziki wa kufoka foka ameweka jina lake.

Kulingana na gazeti la The Independence nchini Uingereza,kitabu hicho kinasema kuwa katika kizazi hiki ,Kanye West ndio mkubwa na vilevile kiongozi wa kidini

Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na vile alivyotufanyia katika maisha yetu''

Kanye West na mkewe Kim Kardashian

Ijapokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu wadhfa huo aliojipatia,amekuwa akijifananisha na Mungu hapo mbeleni.

''Mungu alinichagua mie,alinitengezea njia.Mimi ni chombo cha mungu'',alisema mwaka 2009.

''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja kwa moja''.,aliongezea.

Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni Marilyn Monroe na Michael Jackson.

Tamko la waziri chikawe kuhusu kuzifuta taasisi za kidini na kiraia lapingwa

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe,

Wasomi, wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi katika maeneo mengi nchini, wamepinga vikali tishio la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, la kuzifuta taasisi za kijamii na kidini na kueleza kuwa amekurupuka, hakushauriwa na kushindwa kufuata misingi ya demokrasia na Katiba ya nchi.

Wakizungumza na Gazeti  la  Nipashe, wadau hao walidai kuwa, kufanya hivyo ni kusababisha vurugu na udikteta mkubwa kwa nchi inayoendeshwa kwa misingi ya utawala bora na demokrasia.

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec) na Askofu wa Jimbo la Rulenge, mkoani Kagera, Severin  Niwemugizi, alisema amelipokea tamko hilo kama matamshi ya watu ambao hawajakomaa kisiasa, wasio tayari kupokea maoni ya wengine tofauti na yao na kwamba halina haki bali limejaa woga.

“Katika nchi ya demokrasia yenye viongozi wa namna hii hawana tofauti na madikteta, ukianza kutishia wenzako kuwa ukisema maneno nisiyoyapenda nakufuta huo ni udikteta,” alisema na kuongeza:

“Sheria ya kura ya maoni inasema kutakuwa na makundi ya ndiyo na hapana, najiuliza ni kundi lipi la pande hizo, kwanini wawepo wanaozuiwa wasihamasishe watu kusema hapana kama taasisi za serikali zinazoruhusiwa kuhamasisha ndiyo?” alihoji.

Arusha: Ni  Udikiteta

Baadhi ya asasi za kijamii na watu binafsi mkoani Arusha, walisema tishio hilo ni udikteta ambao ni aibu kutolewa na viongozi katika nchi inayothamini demokrasia na kwamba inapaswa kukemewa kwa vile ina lengo la kupora uhuru wa kujieleza ambao upo kikatiba.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Utetezi wa Haki za Wafugaji, Warina Asali na Waokota Matunda (Pingo’s Forum), Edward Porokwa, alisema kauli ya Waziri Chikawe ni tishio kubwa linalowanyima uhuru wa kujieleza.

“Kweli kauli hii ni tishio kubwa na tunapaswa kuikemea, sababu inatunyima haki na uhuru wa kujieleza kwenye masuala yetu yanayotuhusu kama katiba pendekezwa,” alisema.

Mkurugenzi wa asasi ya Grassroot Youth Development Organisation (GYDO), Henry Cigwasi, alishauri matamko mengine ya viongozi wa serikali yatolewe baada ya kufanyiwa utafiti.

Alisema maisha yote ya binadamu ni siasa, kila kitu anachofanya ni siasa, hivyo hawawezi kuacha kuzungumzia au kutoa elimu ya uraia bila kuzungumzia masuala muhimu yanayohusu maisha yao.

Alisema huku akitoa mfano wa Katiba Inayopendekezwa, kuwa wapo viongozi serikalini ambao wamesikika mara kadhaa wakiwahamasisha wananchi kuipigia kura za ndiyo siku ya kupiga kura ya maoni itakapowadia.

Lakini alisema wapo watu ambao wameichambua Katiba hiyo na kutoa maoni tofauti na viongozi wa serikali, lakini kwa kuwa maoni yao yanakinzana na viongozi wa serikali, wananyamazishwa.

“Kama kuna asasi au taasisi ya dini inatoa elimu kuonya kuhusu ubaya wa kitu fulani, tatizo lipo wapi hapo,” alisema.

Alishauri viongozi wa serikali kabla ya kutoa matamko kuhusu jambo fulani la kitaifa lililotokea basi ni vema kama kungekuwa na majadiliano ya kitaifa na wadau wahusika mapema ili kuepusha kutokea kwa vurugu au shida katika jamii.

Mkazi wa Sakina, Samuel Mollel, alisema hauli hiyo ikitekelezwa italeta vurugu kubwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Dr. Bana: Waziri  Kakurupuka

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema inaonyesha waziri alikurupuka bila kushauriana na kwamba siyo kauli inayopaswa kutolewa kwa umma katika zama hizi za demokrasia na siasa huria.

“Amekosea, ninachojua serikali haiwezi kufuta Katoliki au KKKT, utajiridhisha umewafutia, lakini dini itaendelea kuwapo, askofu hawezi kufuta ukatoliki wangu, hayo yanatokea kwenye mataifa yenye udikteta pekee,” alisema.

Alisema kwa kipindi hiki ambacho waziri alipaswa kusisitiza ni vyama hivyo kuzingatia masharti ya uandikishaji wake bila kutaja siasa.

“Kuanza kusema utavifuta wakati unaona kuna tamko la maaskofu ambalo bado lipo hai ni kujikanganya…akija kwa visivyofuata sheria na Katiba atafikiriwa vibaya,” alisema na kuongeza:

“Ninachoona waziri ali ‘over step’ hakujiridhisha, ndiyo maana serikali zote zinakuwa na msemaji mmoja na siyo kukurupuka, ukishasema unafuta taasisi za dini ni hatari…natoa ushauri wa bure kwa serikali yangu,” alisema.

Mhadhiri mwingine wa Chuo Kikuu cha Dar  es Salaam, Bashiru Ally, alisema: “Jukumu kubwa la serikali yoyote ni katika ‘law and order’ na ‘stability’, lakini serikali ya kidemokrasia haitumii mabavu bali unaweza kujenga amani na utulivu kwenye nchi kwa kujadiliana,” alisema.

Alisema kama zipo sababu za msingi ni vyema mahakama ikatumika kuthibitisha tuhuma zozote kwa kuwa ndicho chombo cha kikatiba chenye uwezo wa kitaalamu wa kusikiliza na kwamba kufuta hivi hivi ni kurudi katika utawala wa kiimla.

THRDC: Tanzania  ya Sasa  Siyo  ya  Zamani

Mtaribu wa Mtandao wa Haki za Binadamu Tanzania  (THRDC), Onesmo Olengurumwa, alisema viongozi wawe makini na kutambua kuwa Tanzania ya sasa siyo ya zamani na kwamba wanapoona mambo hayaendi lazima wazungumze.

Alisema asasi na viongozi wa dini wana wajibu kwenye masuala yote kwa kuwa walishirikishwa kwenye mchakato na Bunge la Katiba, hivyo kwa sasa wanapoona mambo hayako sawa wanapaza sauti.

Alitolea mfano suala la uandikishaji wa wapiga kura kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo wa BVR na mchakato wa kura ya maoni yalikuwa hayakwepeki kuzungumzia kwa kuwa amani ya nchi inategemea masuala yote hayo.

Dodoma:Chikawe  Asitumie  Vibaya  Nafasi  Yake

Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk. Jacob Chimeledya, alisema Waziri huyo asitumie nafasi yake kuchafua zaidi ila kama ni kumsaidia basi Mungu ambariki na wanamuombea.

"Kama atafuta kwa mujibu wa sheria na taratibu na si kama analipuka, atatekeleza kazi yake kwa usahihi, lakini  akilipuka  anaweza kuleta athari kubwa,” alisema.

Alisema hofu yake ni kusiwe na hasira na zikaelekezwa kwa watu wasio na hatia.

"Viongozi wa dini tuna haki  kuelekeza watu kitu gani tunachokifikiri ambacho ni sahihi kwa hiyo kama kuna mtu akitokea akaona ni uasi au si uasi ila na sisi pia tumepewa majukumu ya kumwambia mtu afanye kitu gani ambacho ni sahihi,” alifafanua.

"Hebu tujiulize kwanini huko nyuma haikuwa hivi kwanini hizi hoja kwa sasa zinajitokeza, kwanini leo hii viongozi wa dini wafike kutoa kauli hiyo je, walikuwa ‘right’ au ‘wrong’, haya yanatakiwa kufanyiwa utafiti na ni utafiti rahisi sana,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) mkoa wa Dodoma, Kayumbo Kabutari, alisema Chikawe anadanganya wananchi, nchi haiko salama.

Maaskofu: Tunasubiri  Waraka  wa  Serikali

Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Kanda ya Kaskazini na Kati, Christopher Madilu, alisema tamko ni gumu kueleweka kwa sasa, ingawa viongozi wa dini pamoja na kanisa hilo wanasubiri waraka wa serikali ili watoe msimamo wao.

“Kuna ugumu wake katika kuzungumzia utekelezaji wa tamko la Waziri Chikawe. Sisi tunasubiri waraka wa serikali unaoonyesha kusudio hilo, halafu ndiyo tuzungumze ya kwetu. Lakini mpaka sasa hakuna waraka ulioletwa, inawezekana labda serikali imechunguza na ikaona kuna makosa, hatuwezi kujua kwa hiyo tunasubiri,” alisema Askofu Madilu.

Askofu Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, alisema hawana taarifa na wanasubiri waraka wa serikali.

Prof. Willy Makundi ambaye ni mtaalamu wa mabadiliko ya tabia nchi, alisema anashangazwa na tamko hilo wakati nchi inaongozwa kwa misingi ya sheria na Katiba.

“Hata kama kungekuwa na mtu au kikundi cha watu au taasisi ya dini imevunja sheria, serikali haina nguvu ya kikatiba na ya kiutekelezaji kuyafunga makanisa, isipokuwa mahakama peke yake, kwa sababu ndiyo dalali mkuu wa haki…hakupaswa kutoa vitisho na badala yake angeagiza waburuzwe mahakamani,” alisema Prof. Makundi

Tanga: Serikali  Iache  Vitisho

Baadhi ya wadau wa masuala ya maendeleo mkoani Tanga wameitaka serikali kuacha kutoa vitisho kwa raia wake kwani ni kukiuka Katiba ya nchi kuhusiana na uhuru wa wananchi wa kutoa maoni yao bila kuingiliwa.

Walisema kauli hiyo inaweza kuchangia kusababisha vurugu ndani ya nchi hasa kwa serikali kutaka kutumia mabavu kufanya maamuzi ambayo hayakubaliki, jambo ambalo ni kinyume cha misingi ya utawala bora.

“Utawala bora ni ule unaofuata misingi ya haki na sheria kwa mujibu wa Katiba ya nchi, kama Katiba inayotumika sasa inatambua uhuru wa mwananchi wa kutoa maoni bila kuingiliwa iweje serikali ione ni kosa la jinai,” alisema Mbone Herman, mwanafunzi wa Chuo Kikuu Huria (OUT).

Mariam Said, mkazi wa jijini Tanga, alisema kauli ya serikali inatokana na ukweli kwamba Katiba inayopendekezwa si maoni na mahitaji ya Watanzania, bali ni pendekezwa kwa ajili ya kuwalinda baadhi ya waliopo madarakani.

Mnyika: Nitapeleka  Hoja  Bungeni

Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, John Mnyika, alisema Chikawe angewambia ukweli vyama wanavyotaka kuvifuta ni ambavyo walitangaza kwenye vyombo vya habari na siyo vilivyotoa msimamo katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu.

Alisema iwapo vyama hivyo vitafutwa kwa kisingizio hicho atapeleka hoja bungeni lijadiliwe na waziri awajibishwe.

“Namtaka waziri asijiingize kwenye hatari ya kupelekewa hoja ya kukiuka haki ya kikatiba ya watu kitaasisi kutoa maoni, kama ni suala la watu kutimiza masharti ya kisheria asifute, akifuta nasi tunakwenda kumfuta bungeni,” alisema Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo.
 

“Amekurupuka akasome vizuri Sheria ya Kura ya Maoni ajue ni haki ya watu kushiriki kampeni na kama kura ingekuwa Aprili 30, mwaka huu, kungekuwa na kampeni za ndiyo na hapana,” alisema.

Alisema kauli ya Chikawe na nguvu aliyotumia siyo kura ya maoni pekee, bali wamegundua asasi, taasisi na watu wanataka mabadiliko hawakubaliani na mfumo wa utawala, wanatoa lugha za ukali kuwatisha, kuwaziba midomo kuelekea watu kusaka mabadiliko.

Alisema wanaosababisha kuvunjika kwa amani ni uongozi dhaifu unaoshindwa kusimamia ufisadi na kwamba kinachoonekana kwa sasa ni kuporomoka kwa hali ya maisha ya wananchi na tofauti kubwa kati ya maskini na tajiri ambalo ndilo tishio kubwa.

Kanda  ya  Ziwa  Wamshangaa  Chikawe

Wakazi wa Shinyanga, walisema tamko la Chikawe ni la kukurupuka kutokana na Katiba ya nchi kusema kila mtu ana haki ya kutoa maoni na mawazo yake bila kuvunja sheria za nchi.

Hassani Baruti, mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Shinyanga Mjini, alisema Chikawe amevunja Katiba ya nchi kwa kuingilia uhuru wa mtu binafsi na haiwezekani kuzuia watu kutoa maoni.

Mwanaharakati wa siasa mjini Shinyanga, Saguda Komanya, alisema kila nchi ina miongozo yake na katika suala la Katiba inayopendekezwa kila mtu ana wajibu wa kuikosoa na kuitolea maoni.

Komanya alisema suala la hofu ya amani kuelekea uchaguzi mkuu halipo isipokuwa Jeshi la Polisi linatakiwa lisiegemee upande wa chama chochote zaidi ya kutenda haki.

 Mkoani Simiyu, baadhi ya asasi zimeleeza kushangazwa na tamko hilo na kulitiliwa hofu.

 Mwenyekiti wa mtandao wa asasi za kiraia wilayani Maswa, Nicodemas Lutta, alisema kitendo cha Chikawe kutoa tamko hilo ni kuwanyima wananchi pamoja na asasi zao haki ya kidemokrasia ya kuamua mambo nchini.

Alisema kuzifungia asasi za kiraia na kidini kuna utaratibu wake, na kumtaka Chikawe atoe ushahidi wa asasi zinazotuhumiwa kuliko kujumuisha asasi zote hususani zile za kidini.

Lutta alisema haiwezekani kutenganisha siasa na dini na kuhoji serikali imekuwa ikiwahimiza viongozi wa madhehebu ya dini kuhubiri amani na upendo hasa kuelekea uchaguzi mkuu na kuwahimiza wananchi wao bila kujali imani zao za kidini kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa.

“Kwanini nawakataza wasihamisishe kupigia kura ya hapana wakati Katiba ni ya wananchi?” alihoji.

 Wilayani Chato baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini, walisema ni lazima kauli hiyo aifute kwani inaweza kusababisha machafuko.

“Chikawe lazima atambue viongozi wa dini ni walinzi wakubwa wa amani nchini, hivyo kitendo cha kuwataka kuwazuia kutoa maoni yao wakati muelekeo wa nchi unaenda mrama hakiwezekani,” alisema mchungaji wa kanisa Anglikana Chato, Zacharia Samson.

Katibu wa Chadema wilayani Chato, Mange Ludomya, alisema Chikawe amekiuka katiba ya nchi kwa kumkataza mtu kutoa maoni yake bila kuvunja sheria za nchi.

“Hivyo ni vitisho ili kuwafanya wananchi waikubali Katiba inayopendekezwa isiyoonyesha dira kwa Watanzania katika miaka 50 ijayo,” alisema Emmanuel Magida mkazi wa Igoma, jijini Mwanza.

Edward Mboje mdau wa asasi za kiraia, alisema waziri huyo hakutumia busara katika tamko lake hilo kwani asasi siyo serikali bali ni wananchi, hivyo haina haja kutoa kauli inayowanyima wananchi haki ya kutoa maoni kwa mambo ya kisimingi

Wageni waendelea kushambuliwa A kusini

Raia wa kigeni ashambuliwa Afrika Kusini

Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.

Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kutawanya umati kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa moto.

Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda baadaye.

Maandamano ya kupinga uvamizi wa wageni

Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu watano wameuawa.

Rais Jacob Zua amelaani ghasia hizo na maandamano ya amani mjini Durban siku ya Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu kumi.

Breaking news:19 wafa kwa ajali ya gari mbeya

Watu wapatao 19 wamekufa katika ajali ya gari ndogo aina ya hiace iliyotokea kiwira jijini mbeya ambapo gari hiyo iliingia kwenye mto uliopo pembezoni mwa mto huo habari zaidi endelea kua nasi

Hizi ndizo nauli mpya za Mabasi Tanzania

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi kavu jana imetangaza nauli mpya za usafiri ambapo Mabasi ya abiria ya masafa marefu nauli zake zikipungua huku daladala nauli zikibaki vile vile. 

Akitangaza Viwango hivyo vipya vitakavyoanza kutumika tarehe 30 mwezi huu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA Gilliadi Ngewe alisema baada ya mchakato wa kupanga bei kukamilika, bei za mabasi ya Masafa ya mbali zimeshuka kwa asilimia 5.8 hadi 7.8 kwa kilometa kulingana na daraja la basi.
  
Ngewe amesema kuwa mabasi ya daraja ya chini yamepungua kutoka shilingi 34.8 hadi 34 kwa kilometa, Daraja la kawaida toka shillingi 46.1 hadi 42.5 kwa kilometa na daraja la kati toka shilingi 53.2 hadi 50.1 kwa kilometa huku dalalada zikishuka kwa shillingi 23 lakini kwa usumbufu wa chenji Nauli zitabaki vile vile.
  
Kwa Upande wa wamiliki wa daladala kupitia kwa mwenyekiti wao Sabri Mabrouk wao wanataka nauli iongezeke toka 400 ya sasa mpaka 600.

------

TAARIFA KWA UMMA

NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU NA MIJINI

1.0 UTANGULIZI

Kuelekea mwishoni mwa mwaka 2014 bei ya mafuta yatumikayo katika vyombo vya usafiri wa abiria nchini ilianza kushuka. Kufuatia kushuka huko kwa bei, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ilikuwa ikipokea wito wa kupitia upya viwango vya juu vya nauli ambavyo viliwekwa na Mamlaka mwezi Aprili, 2013. Hivyo SUMATRA ikaamua kuandaa mikutano ya wadau kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu haja ya kurekebisha viwango vya nauli zilizopo.

Aidha, tarehe 09 Machi, 2015, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma Zinazodhibitiwa na SUMATRA (SUMATRA Consumer Consultative Council (SCCC)) liliwasilisha kwa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) maombi ya kushusha nauli za mabasi ya masafa marefu na mijini. Katika maombi hayo Baraza liliainisha sababu za kuomba punguzo hilo kuwa ni kushuka kwa bei za mafuta na kodi ya forodha kwa mabasi mapya kutoka asilimia 25 hadi 10; punguzo hilo lilianza Julai, 2014.

1.1 MAOMBI

Usafiri wa Mijini: Katika usafiri wa mijini, maombi yalikuwa ni kupunguza nauli kwa asilimia 25; hivyo kwa njia yenye umbali wa kilomita 10, nauli iliyopo sasa ya TZS 400 ilipendekezwa kushushwa hadi kufikia TZS 300.Usafiri wa Masafa Marefu:Maombi yalikuwa ni kushusha nauli iliyopo kwa kilometa moja anayosafiri abiria katika basi la kawaida kutoka TZS 36.89 hadi TZS 28.05; punguzo la asilimia 23.96. Aidha, kwa basi la hadhi ya juu (luxury bus) kushusha kutoka TZS 58.47 hadi TZS 47.19; punguzo la asilimia 19.29.

2.0 UTARATIBU WA KUFANYA MAPITIO YA NAULI
SUMATRA iliyafanyia kazi maombi hayo kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Sheria ya Bunge Na.9 ya Mwaka 2001, na Kanuni za Tozo za Mwaka 2009 ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma, watumiaji wa huduma pamoja na wananchi kwa ujumla ili kupata maoni yao. Ushirikishwaji huo ulifanywa kupitia mikutano iliyofanyika tarehe 9 Machi, 2015 Mkoani Mwanza; tarehe 12 Machi, 2015 Mkoani Kigoma; na tarehe 18 Machi, 2015 Jijini Dar es Salaam. Maoni yaliyotolewa katika mikutano hiyo yalizingatiwa katika tathmini na Mamlaka. 

Taarifa ya tathmini na mapendekezo ya viwango vipya vya nauli iliwasilishwa kwa Bodi ya Wakurugenzi ya SUMATRA kwa ajili ya maamuzi.

3.0 NAULI ZA MIJINI
Bodi ya Wakurugenzi ya SUMATRA ilikutana Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Aprili, 2015 ili kupitia taarifa ya tathmini na mapendekezo ya viwango vya nauli kwa ajili ya maamuzi.

3.1 Masuala Yaliyobainika
Kufuatia tathmini iliyofanywa ya usafiri wa mijini, BODI ilibaini kwamba:Bei ya mafuta ilikuwa imeshuka ikilinganishwa na bei iliyokuwepo wakati viwango vilivyopo sasa vilipoanza kutumika Mwezi Aprili, 2013; ambapo kwa wastani bei ya lita ya dizeli iliuzwa TZS 2,071.67 kufikia Machi, 2015 wastani wa bei ya Dizeli kwa lita katika vituo ulishuka mpaka TZS 1,665.38; mwezi Aprili, 2015 bei ya wastani ilipanda kufikia TZS 1,779.57.Mwenendo wa bei za mafuta kufikia Aprili, 2015 unaonyesha kuwa bei ya mafuta imekuwa ikibadilikabadilika na kwamba kulikuwa na uwezekano wa bei kupanda.Gharama za mafuta zilikuwa muhimu kuzingatiwa pamoja na gharama nyinginezo, ambazo zilifikia asilimia 70 ya gharama za uendeshaji.Kulikuwa na mabadiliko katika viashiria vya kiuchumi kama vile mfumuko wa bei na thamani ya shilingi na mabadiliko hayo yalipaswa kuzingatiwa katika kukokotoa viwango vya nauli.Punguzo la ushuru wa forodha kwa uagizaji wa mabasi mapya ulikuwa na faida katika kuchochea uingizaji wa mabasi mapya nchini ili kuboresha hali ya usafiri nchini. Hata hivyo sehemu kubwa ya mabasi yaliyopo nchini kwa sasa hayakupata punguzo hilo kwa kuwa yaliingizwa kabla ya Julai, 2014 punguzo hilo lilipoanza kutumika.Mazingira ya uendeshaji na utoaji huduma za usafiri mijini yanapaswa kuzingatiwa ili kufikia viwango vya nauli ili kuifanya huduma ya usafiri kuwa endelevu. Kwa upekee, ongezeko la msongamano wa magari mijini na athari zake katika utoaji wa huduma za usafiri mijini zinapaswa kuzingatiwa.Gharama za utoaji huduma za usafiri mijini zinapaswa kutazamwa kwa ujumla wake, ikiwa ni pamoja na punguzo la bei ya mafuta, ili kufikia viwango vya nauli vinavyostahili.Baada ya kuzingatia vigezo muhimu katika ukokotoaji wa nauli, punguzo lililojitokeza katika viwango vya nauli kikomo ni kama inavyobainishwa hapa chini: 

Viwango Vya Nauli Kutokana na Ukokotoaji

Njia

Nauli ya Sasa

Nauli iliyokokotolewa

%

0 - 10 km (+CBD)

400

376.77

5.8

11 - 15 km

450

448.62

0.3

16 - 20 km

500

485.34

2.9

21 - 25 km

600

583.34

2.8

26 - 30 km

750

742.74

1

3.2 Maamuzi ya BODI

Baada ya kutafakari viwango vilivyotokana na ukokotoaji uliozingatia masuala muhimu yaliyoainishwa, BODI imeridhia viwango vya nauli vilivyopo sasa kuendelea kutumika.

Uamuzi huu unatokana na punguzo lililokokotolewa Kuwa dogo ikilinganishwa na viwango vilivyopo sasa. Aidha, viwango vilivyokokotolewa iwapo vitapitishwa vitasababisha usumbufu katika malipo.

Viwango vya Nauli Mpya kwa Watu Wazima
Viwango vipya vya nauli kikomo vya mabasi ya mjini vilivyoridhiwa kwa watu wazima ni kama ifuatavyo: 

Viwango Vya Nauli Mjini Vilivyoridhiwa

Njia

Nauli ya Sasa

(TZS)

Viwango Vilivyoridhiwa

(TZS)

0 - 10 km (+CBD)

400

400

11 - 15 km

450

450

16 - 20 km

500

500

21 - 25 km

600

600

26 - 30 km

750

750

Viwango vya Nauli Mpya kwa Wanafunzi 
BODI imeamua kuwa nauli ya mwanafunzi nayo ibaki kama ilivyo nauli ya sasa ambapo mwanafunzi analipa TZS 200.

VIWANGO VYA NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU
BODI ilipokea tathmini kuhusu nauli za usafiri wa masafa marefu.

4.1 Masuala Yaliyobainika
Kufuatia tathmini iliyofanywa ya nauli kikomo za usafiri wa masafa marefu, BODI ilibaini kwamba:Bei ya mafuta ilikuwa imeshuka ikilinganishwa na bei iliyokuwepo wakati viwango vya sasa vilipoanza kutumika Mwezi Aprili, 2013; ambapo kwa wastani bei ya lita ya dizeli iliuzwa TZS 2,071.67 kufikia Machi, 2015 wastani wa bei ya Dizeli kwa lita katika vituo ulishuka mpaka TZS 1,665.38; mwezi Aprili, 2015 bei ya wastani ilipanda kufikia TZS 1,779.57.Mwenendo wa bei za mafuta kufikia Aprili, 2015 unaonyesha kuwa bei ya mafuta imekuwa ikibadilikabadilika na kwamba kulikuwa na uwezekano wa bei kupanda.Gharama za ununuzi wa mafuta zilikuwa muhimu kuzingatiwa pamoja na gharama nyinginezo, ambazo zilifikia asilimia 70 ya gharama za uendeshaji.Kulikuwa na mabadiliko katika viashiria vya kiuchumi kama vile mfumuko wa bei na thamani ya shilingi na kwamba mabadiliko hayo yalipaswa kuzingatiwa katika kufikia viwango vya nauli.Punguzo la ushuru wa forodha kwa uingizaji wa mabasi mapya lilikuwa na athari chanya katika kuchochea uingizaji wa mabasi nchini. Hata hivyo sehemu kubwa ya mabasi yaliyopo nchini kwa sasa hayakupata punguzo hilo kwa kuwa yaliingizwa kabla ya punguzo hilo kuanza kutumika.Katika ukokotoaji wa nauli ni muhimu kuzingatia madaraja ya mabasi kama yalivyoelekezwa katika Kanuni za Huduma za Abiria, 2014 (The Road Transport (Passenger Service) Regulations, 2014 zinazoainisha madaraja manne ya mabasi;daraja la kawaida la chini, daraja la kawaida la juu, daraja la hadhi ya kati na daraja la Juu.Gharama za utoaji huduma za usafiri kwa ujumla wake zinapaswa kuzingatiwa kwa madaraja mbalimbali ili kufikia viwango vya nauli vinavyostahili.Udhibiti wa nauli unapaswa kujielekeza katika madaraja matatu yafuatayo: (1) daraja la kawaida la chini, (2) daraja la kawaida la juu na (3)daraja la hadhi ya Kati ili kutimiza wajibu wa kuwalinda watumiaji wenye kipato cha chini.

4.2 Maamuzi ya BODI
Baada ya kutafakari tarifa iliyowasilishwa BODI iliridhia viwango vipya vya juu vya nauli kwa mabasi ya masafa marefu kuwa kama vinavyoonyeshwa hapo chini: 

Viwango Vipya vya Nauli za Mabasi ya Masafa Marefu

Daraja la Basi

Nauli ya Sasa

(TZS/Abiria/Km)

Viwango Vipya vya Nauli Vilivyoridhiwa

(TZS/Abiria/Km)

Daraja la Kawaida la Chini

(Lower Ordinary bus -Lami

36.89

34.00

Daraja la Kawaida la Chini

Lower Ordinary Bus) - Vumbi

46.11

42.50

Daraja la Kawaida la Juu

(Upper Ordinary Bus)

-

44.96

Daraja la Kati

(Semi-Luxury Bus)

53.22

50.13

BODI pia imeamua kwamba nauli za mabasi ya hadhi ya juu ( luxury bus) hazitadhibitiwa ili kuchochea ubunifu katika utoaji huduma na ushindani kati ya huduma za barabara na njia nyinginezo za usafiri.

Mamlaka imeandaa majedwali ya nauli kwa kuzingatia viwango vipya. Majedwali hayo yanaweza kupatikana katika tovuti ya Mamlaka www.sumatra.go.tz.

HITIMISHO

Viwango hivi vipya vinapaswa kuanza kutumika siku 14 baada ya taarifa kutolewa kwa umma. Hivyo basi viwango hivi vitaanza rasmi tarehe 30 Aprili, 2015.

Wamiliki wa mabasi pamoja wafanyakazi wao wanaagizwa kutoza viwango vya nauli vilivyoridhiwa na Mamlaka.

Aidha, abiria na wananchi kwa ujumla wanahamasishwa kutoa taarifa SUMATRA kupitia namba za simu za bure ambazo ni 0800110019 na 0800110020 pale wanapotozwa nauli ya juu zaidi ya nauli kikomo iliyoridhiwa.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu

SUMATRA

15 Aprili, 2015

Alhamisi, 16 Aprili 2015

Mtoto aanguka kutoka ghorofa ya tano jijini Dar

Katika hali hisiyo ya kawaida, mtoto mmoja ambaye jina lake halijafahaamika ameanguka mchana wa leo kutoka juu ya jengo la ghorofa, ghorofa ya tano, huko maeneo ya kota za jeshi, Mwenge Maghorofani..

Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia tukio hilo wameelea kuwa, mtoto huyo hadi sasa ameumia vibaya sehemu za kichwani na kutoka damu nyingi, ambapo awali alikimbizwa hospitali ya Lugalo na baadaye amepelekwa Muhimbili.

 kwa taarifa zaidi tutawaletea

chanzo-Eddy blog

Wenger:Walcot haondoki Emirates

Walcott na mkufunzi Arsene Wenger

Meneja wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger ana imani kwamba Theo Walcot ataweka mkataba mpya na kilabu hiyo ya Ligi ya Uingereza.

Walcot mwenye umri wa miaka 26 amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na anahusishwa na uhamisho wa kujiunga na kilabu ya Liverpool.

Alipoulizwa kuhusu kusalia kwa Walcot katika uwanja wa Emirates,Wenger alisema kuwa nina imani kuwa Walcot ana maisha mazuri mbeleni.

Mshambuliaji huyo ameanza mechi tano pekee msimu huu huku akiendelea kuuguza jeraha la mguu alilopata msimu uliopita.

Lakini mchezaji huyo wa Uingereza ambaye amefunga mabao 77 katika mechi 203 alizochezea Arsenal huenda akajumuishwa katika kikosi cha mechi ya semi fainali ya kombe la FA dhidi ya Reading.

''Amerudi kutoka katika jeraha baya sana na kila wiki anaimarika'',Wenger alisema.

Jumatano, 15 Aprili 2015

Mda wa kupiga kura waongezwa sudan

Uchaguzi nchini Sudan

Tume ya uchaguzi nchini Sudan inasema kuwa imeongeza mda wa kupiga kura ya urais na ubunge hadi siku ya alhamisi huku ripoti za idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza zikitolewa.

Kura hiyo imesusiwa na upinzani ambao unasema kuwa idadi hiyo ya wapiga kura inaonyesha raia hawajali na kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba rais Omar Al Bashir atatangazwa mshindi.

Bwana Al Bashir amekuwa mamlakani tangu mwaka 1989.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir

Shughuli ya upigaji kura ilitarajiwa kuchukua siku tatu na kukamilika leo.

Mkuu wa tume ya uchaguzi alisema kuwa alitarajia idadi ya wapiga kura ijitokeze na kufikia asilimia 45.

Azam yaipa Yanga nafasi ya ubingwa

Yanga kwa raha zao

Kicheko kinaendelea kutawala katika klabu ya Yanga baada ya sare kuendelea kuitesa Azam FC katika mechi ya tatu mfululizo hivyo kuipa Yanga nafasi ya ubingwa.

Azam , katika mechi ya leo iliyochezwa mkwakwani mjini Tanga, imetoka droo ya 0-0 na wenyeji Mgambo Shooting.

Katika mechi iliyopita, mabingwa hao watetezi walitoka sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar, ikiwa ni juma moja tu baada ya kutoka sare ya 1-1 na Mbeya City.

Sare hizo zinaipa Yanga nafasi ya ubingwa kwa tofauti ya pointi 7.

Kocha was Yanga, Hans Pluijm amenukuliwa name vyombo vya habari akisema, anahitaji mechi tano tu kushinda ili kuwa mabingwa.

Yanga, ikiwa na kibarua cha mechi ya Shirikisho barani Afrika dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia hapo Jumamosi jijini Dar es Salaam, inaongoza ligi ikiwa na pointi 46 katika mechi 21 ilizocheza wakati Azam inafuatia ikiwa na pointi 39.

Logo hiyo inaelekea ukingoni kuisha hapo mwezi Mei

Mali za gwajima zaanikwa yasemekana ndie mchungaji tajiri Africa

Sakata la Gwajima limechukua sura mpya baada ya mchungaji huyo kutakiwa na jeshi la polisi kupeleka nyaraka mbalimbali zinazohusu umiliki wa mali zake!

Mchungaji Gwajima katika kupingana na amri hiyo halali ya jeshi la polisi, amekimbilia kwa mawakili, ili tu kuweka pingamizi la yeye kuthibitisha umiliki wake wa mali alizonazo na namna alivyozipata.

Itakumbukwa kuwa jeshi la polisi lilimtaka Gwajima apeleke nyaraka zifuatazo: Hati ya usajili wa kanisa lake, namba ya usajili wa kanisa lake, hati ya umiliki wa helikopta, hati za nyumba anazomiliki, idadi ya makanisa yaliyopo chini yake na taarifa za mapato na matumizi ya makanisa yake.

Nyaraka zingine ni: majina ya bodi ya udhamini wa kanisa na waraka wa maaskofu uliosomwa makanisani ambao Kardinali Pengo aliupinga!

Taarifa kuhusu mali za Gwajima ni hii hapa:

...Gwajima ana miliki nyumba nne za ghorofa Mbezi beach na kwa mujibu wa ripoti ya uthamini wa nyumba hizo jumla zina thamani ya bilioni 11 na milioni 400 (11.4 bilioni) pesa za Kitanzania.

...Pia ana nyumba nyingine kadhaa kwenye maeneo mbalimbali nchini ila hadi hivi sasa taarifa za uhakika za thamani ya nyumba hizo bado hazipo wazi.

...Gwajima ana miliki helikopta moja na magari ya kifahari kama vile Hammer, Range rover. Magari mengine ni Nissani Murano, Land Rover 4 na Land Cruiser V8.

...Gwajima pia amenunua magari mengine 40 yenye thamani kati ya Tshs 10 milioni na Tshs 20 milioni na kuwapatia wachungaji wake kote nchini kwa ajili ya shughuli zao binafsi na magari yote hayo yapo chini ya umiliki wake.

...Inakadiliwa kuwa akaunti binafsi za Gwajima zilizopo hapa nchini zina zaidi ya Tshs 20 bilioni ikiwa ni fedha zilizopo nje ya fedha za akaunti ya kanisa.

Aidha, pamoja na yeye mwenyewe kutaarifu juu ya mali zake kama ambavyo zimeorodheshwa hapo juu, lakini siku ya jana akiwa anahubiri kanisani kwake alikana kuwa yeye sio tajiri! 

Gwajima alikaririwa akisema kwamba mali zote anazomiliki ni baraka tu za Mungu na sio kwamba yeye ni tajiri. Gwajima alisisitiza kuwa yeye ni maskini kama walivyo maskini wengine wakiwemo wahumini wake, na wanaosema yeye ni tajiri wanawivu na wanamuonea. 

Jumanne, 14 Aprili 2015

Obama kuiondoa Cuba kwenye orodha ya ugaidi


Rais Barack Obama (kulia) na Rais Raul Castro wa Cuba (kushoto)

Rais Barack Obama amesema ataiondoa Cuba kutoka orodha ya Marekani ya nchi zinazofadhili ugaidi duniani.

Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani imesema hatua hiyo inakuja huku kukiwa na jitihada za kujenga uhusiano kati ya Marekani na Cuba.

Uwepo wa Cuba katika orodha hiyo pamoja na nchi za Syria, Iran na Sudan kilikuwa kigezo cha Cuba katika mazungumzo yake na Marekani ya kufungua ofisi za balozi kati ya nchi hizo.

Seneta wa chama cha Republican Marco Rubio ameishutumu Ikulu ya Marekani kwa uamuzi huo, akisema kuwa Cuba bado ni taifa linalofadhili ugaidi.

"Wanawahifadhi Wamarekani ambao wanakimbia mkono wa sheria, akiwemo mtu aliyemuua afisa wa polisi huko New Jersey zaidi ya miaka 30 iliyopita," amesema Bwana Rubio, Mmarekani mwenye asili ya Cuba ambaye alizindua kampeni yake ya uchaguzi wa rais wa Marekani 2016.

"Ni nchi ambayo pia inaisaidia Korea Kaskazini kukwepa vikwazo vya silaha vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa."

Bwana Obama alitangaza tukio la kihistoria la kurejesha uhuasiano kati ya Marekani na Cuba mwezi Desemba 2015 lakini vikwazo vya kibiashara vya Marekani dhidi ya Cuba vinabakia, na vinaweza kuondolewa tu na baraza la Congress.

Kundi la Al-shababi latoa tamko kuhusu kuvamia Tanzania

TAARIFA KUTOKA REDIO YARAT FM YA SOMALIA LEO SAA mbili asubuhi kwenye kipindi cha MAKHAR TWALLIB:

 Mkuu Wa kikundi cha AL shabab Leo asubuhi wakati akihojiwa juu ya taarifa zilizoenea kwamba wana mpango Wa kuvamia Tanzania amesema haya yafuatayo.

 Kamwe hawajawahi kufikiria kushambulia Tanzania Kwa sababu hawana sababu ya kufanya hivo!

 Amesema kwamba mbali ya kuzingatia kuwa 

 

Tanzania kuna waislam wengi Bali pia wanajua na kutambua msaada Wa mwalim Julius kambarage nyerere mwaka 1995 alipotoa msaada Wa tani 500000 za mahindi kipindi nchi hiyo ina janga LA njaa.Hivyo hawawezi kulipa unyama chuo Kwa marehemu baba Wa taifa.

Pia kiongozi huyo aliongeza kuwa Tanzania haijapeleka jeshi lake somalia yenyewe nchi kama nchi tofauti na Kenya na Uganda. Wanajeshi wachache watanzania walioko somalia ni katika jeshi LA AU na sio Kwa amri ya Tanzania.

Kiongozi huyo pia katoa pole katika muda Wa siku mbili ambao watanzania hususani wanachuo waliokuwa katika hali ya sintofahamu na pia vyombo vya usalama ambavyo vililazimika kuimarisha ulinzi katika sehemu nyeti mbali mbali.

Kiongozi huyo kamaliza Kwa kusema kwamba wao wanazingatia msemo Wa Quran kwamba,"Fight those who fight you,spare those who don't fight you'

Mama yake Beyonce aolewa

Maharusi Tina na Richard Lawson

Mamake Beyonce Knowles,Tina 61,ameolewa kwa mara ya pili .

Tina aliolewa na mchumbake wa siku nyingi msanii Richard Lawson, mwenye umri wa miaka 67.

Wawili hao walifunga pingu za maisha katika boti moja la kifahari karibu na ufukwe wa Newport California.

Wanawe Beyonce na Solange walishuhudia ndoa hiyo

Beyoncé na mumewe Jay Z walikuwepo kushuhudia ndoa ya bi Tina.

Dadake Beyoncé Tina, Solange pia alikuwepo katika hafla hiyo ya kufana.

Mumewe Richard anakumbukwa kwa mchango wake katika riwaya ya ''All My Children'', iliyosimulia msiba wa mwaka wa 1982 wa Poltergeist.

Bwana na Bi Harusi Tina na Richard Lawson

Imekuwa ni msimu wa baraka kwa familia ya bi Tina ambaye majuzi tu alishuhudia ndoa ya mwanawe Solange na promota wa muziki Alan Ferguson mwisho wa mwaka uliopita.

Haijabainika iwapo baba yao mzazi ambaye pia aliwahi kuwa meneja wa beyonce' bwana Mathew Knowles alikuwepo.

Tina na Mathew Knowles katika ndoa yao ya awali

Mathew, 63, aliishi na Tina kwa miaka 31 kati ya mwaka wa 1980 na 2011 na walijaaliwa watoto wawili Beyonce na Solange.

Baada ya wawili hao kutofautiana Mathew alimuoa bi Gena Charmaine mwaka wa 2013 huko Houston, Texas Marekani..

Al-shababi waua watu 9 somalia


Wavamizi walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo kabla ya wavamizi kuingia wakiwa wamejihami kwa bunduki

Watu 9 wameripotiwa kuuawa katika majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia.

Mwandishi wa BBC Ibrahim Aden,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo

kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.

Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab,

amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa

''wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara ya elimu''

Mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa polisi.

Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde.

Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu

Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .

Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo.

hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo .

Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.

Iran yakomesha ibada ya Umra Makka

Iran yakomesha Hija ya Umra Mecca na Medina

Huku uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia, ukiendelea kusambaratika, kuhusiana na mzozo wa kisiasa nchini Yemen,

Utawala wa Tehran, umetangaza kusitisha safari zote za hija kuelekea Mecca na Medina.

Kwa mujibu wa serikali ya Iran, raia wa nchi hiyo hawataruhusiwa kuelekea Saudia kwa maadhimisho ya Umrah,

kufuatia kudhulumiwa kwa wanaume wawili, raia wa nchi hiyo, wakati walipokuwa wakirejea nyumbani katika uwanja wa Jedda, mwezi uliopita.

Kashfa hiyo iliyohusiana na mzozo wa ngono na maswala ya kidini umepalia makaa katika mgongano wa kisiasa katika ya mataifa hayo mawili hasimu katika eneo la mashariki ya kati.

Mamia ya wairan waliandamana hadi nje ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran wakitaka serikali ya taifa hilo kushinikiza

Saudia kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya watuhumiwa wa kashfa hiyo ya ngono.

Waziri wa turathi za taifa wa Iran Ali Jannati, amesema kuwa serikali ya Saudia imewatia mbarani watuhumiwa hao.

Takriban raia nusu milioni wa Iran huzuru Saudi Arabia kila mwaka kuadhimisha Umrah

Tehran na Saudia Arabia zinaunga mkono pande hasimu katika vita vinayoendelea huko Yemen na ilikuwa inatarajiwa kuwa raia wachache mno wa Iran watasafiri kuhiji mjini Mecca.

Jumapili, 12 Aprili 2015

Man u yaipiga Man city 4-1

Manchester United ilipanda tena katika nafasi ya tatu katika jedwali la ligi ya Uingereza ikiwa pointi moja nyuma ya Arsenal baada ya kuwacharaza mahasimu wao wa jadi Manchester City mabao 4-2.

Sergio Aguerro alikuwa wa kwanza kuiweka City kifua mbele lakini vijana wa Old Trafford walisawazisha kupitia Ashley Young .

Kocha Pelegrini

Maruane Fellaini alifunga kichwa kizuri kilichoiweka Manchester United kifua mbele kabla ya kiungo wa kati Juan Mata kufunga bao zuri.

Chris Smalling alipiga kichwa kisafi kilichomwacha kipa wa City bila jibu kabla ya Aguero kufunga bao la kufutia machozi na la pili kwa upande wa City ambo kwa sasa wamepoteza mechi sita kati ya nane walizocheza.

Wachezaji wa manchester city

Katika mechi ya mapema viongozi wa ligi Chelsea waliendelea na matokeo mazuri baada ya kuwachapa wenyeji wao QPR bao 1-0.

Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas ndiye aliyefunga bao hilo la pekee.

Nelly mashakani kwa Dawa za kulevya

Mshindi wa tuzo ya Grammy mwanamuziki Cornell Haynes ama kwa jina maarufu Nelly amekamatwa na shtaka la mihadarati baada ya polisi kusimamisha basi alilokuwa akisafiria mjini Tennessee nchini Marekani.

Alikamatwa kwa kuwa basi hilo halikuwa na vibandiko halali kabla ya kuchunguzwa kutokana na harufu ya bangi iliokuwa ikinuka.

Idara ya usalama na usalama wa nyumbani baadaye ilisema kuwa Nelly alipelekwa hadi Jela ya kaunti ya Putnam baada ya basi hilo kusimamishwa.

Msanii huyo wa muziki wa kufokafoka alishtakiwa na makosa ya kumiliki bangi kabla ya kuachiliwa kwa dhamana .

Mtu mwengine ambaye pia alikuwa akiabiri basi hilo alikamatwa na kushtakiwa ,mamlaka imesema.

Alhamisi, 9 Aprili 2015

Tenga auchinja CAF

Leodgar Chilla Tenga mjumbe wa kamati ya utendaji ya CAF

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).

Aidha Rais Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA.

Katika salamu hizo na nakala zake kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter, Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na kwa ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.

Tenga amechaguliwa nafasi hiyo baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote wanachama wa CECAFA.

NB: Kesho alhamisi saa 5 kamili asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TFF uliopo Karume, makocha wa Twiga Stars na She-Polopolo wataongelea maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa siku ya ijumaa.

Jumatano, 8 Aprili 2015

Maombolezo yafikia tamati Kenya

Kulikuwa na kaburi la muda,misalaba na mishumaa vilivyowekwa katika viwanja vya mji mkuu wa Kenya ,Nairobi ili kuwakumbuka wanafunzi waliouawa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa ,shambulio ambalo lililotekelezwa na mwanamgambo aliyekuwa na silaha kutoka katika kundi la Al Shabaab,mwishoni mwa wiki iliyopita.

Picha za waathirika wa shambulio hilo wapatao mia moja na arobaini na nane ziliwekwa bayana katika ibada ya mkesha, katika maadhimisho ya kuhitimisha maombolezo ya kitaifa nchini humo yaliyodumu kwa muda wa siku tatu.

Ni huzuni,kupoteza wapendwa wangali wachanga.

Waandaji wa mkesha huo waliwataka waombolezaji waliokuwa tayari kuhudhuria ibada hiyo, kuvaa mavazi meusi,na pia kubeba maua ridi . Mapema,wanachuo kutoka chuo cha Garissa waliandamana katika mji mkuu wa Nairobi,huku wakiwa na ujumbe wenye kuitaka serikali ya Kenya kuimarisha ulinzi nchini humo.

Garissa kwenyewe watu wapatao elfu mbili walikusanyika katika mkutano wa hadhara ,nayo mahakama kuu mjini Nairobi imetoa mwezi mmoja zaidi kwa polisi kuwahoji washukiwa sita wa tukio la Garissa ambao wanashukiwa kuwapelekea silaha wauaji waliotekeleza tukio lile.

Rand paul atangaza nia

Seneta kutoka Kentucky wa chama cha Republican Rand Paul, ametangaza nia rasmi, kuwa atagombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Marekani.

Paul ameyasema hayo wakati wa kampeni zake anazoziendesha kupitia tovuti yake, na amenukuliwa kuwa anataka kuirejesha nchi hiyo katika kanuni uhuru na serikali ndogo.

Kampeni zake alizindulia katika jimbo la Louisville mapema wiki hii. Rand Paul ameungana na seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz, katika harakati hizo ambazo zimevuta hisia za nusu ya wagombea wakubwa wa chama cha Republican,na hii ni pamoja na gavana wa zamani wa jimbo la Florida Jeb Bush,gavana wa Wesconsin Scott Walker,ambaye bado hajatoa tamko lake rasmi.

Jumanne, 7 Aprili 2015

Mtoto azaliwa bila Pua

Eli Thompson alizaliwa tarahe nne Machi jioni, lakini alikuwa na kasoro moja, hakuwa na pua.

Siku niliyojifungua, kila kitu kilikuwa sawa.'' Mamake Brandi McGlathery ameambia ABC News Today nchini Marekani.

''Alipozaliwa daktari alimweka kifuani mwangu. Nilipomwangalia kwa karibu, nilisema ' Hana pua'. Walimchukua na kutoka naye.

McGlathery amesema kwamba daktari alikaa kando ya kitanda chake ili kumweleza hali ya mtoto wake. ''Alikuwa amehuzunika..''Amesema.'' Nilijua papo hapo kuwa hakuwa sawa.''

Hata ingawa mtoto wake hakuonyesha kasoro zozote zaidi, McGlathery amesema kuwa alishangazwa na kuhuzunika kutokana na habari hizo.

Lakini licha ya kukosa pua, Brown amesema kuwa mtoto huyu ana afya nzuri na pia ni mtoto mrembo.

Jumatatu, 6 Aprili 2015

Akon awashusha wanamziki wa Kenya

Mwanamuziki mwenye tuzo la kimataifa Akon amesema kuwa hakuna hata mwanamuziki mmoja wa Kenya ambaye amemuomba kufanya naye 'kolabo'mara zote tano ambazo ameweza kuzuru Kenya.

Akon Hatahivyo ameliambia jarida la Mondayblues nchini Kenya kwamba wasanii wa muziki barani Afrika pia wanafaa kuimarisha viwango vyao ili kutoa changomoto kwa wasanii kama yeye ili kuweza kushirikiana nao.

Tamko la msanii huyo linajiri kufuatia madai kutoka kwa wanamuziki wa Kenya kwamba hayuko tayari kufanya nao Kazi.

Jumapili, 5 Aprili 2015

Papa awafanyia maombi wanafunzi waliouwawa Kenya

Papa Francis amewasalia hadharani wanafunzi wa Kenya waliouwawa Alhamisi.

Akitoa ujumbe wake wa pasaka mbele ya umati mkubwa katika medani ya Saint Peter's, Vatican, Papa Francis alitoa wito kwa mateso dhidi ya Wakristo dunia nzima kukomeshwa.

Kiongozi huyo wa kidini anayewaongoza karibia wafuasi billioni 1.2 wa kanisa katoliki alipinga yale yanayoendelea mashariki ya kati na kwengineko lakini akitumai kwamba makubaliano ya mpango wa nyuklia nchini Iran ni hatua muhimu ya kuimarisha usalama duniani.

Kabla ya kuanza mahubiri yake, Papa alikwenda kwenye medani kuwalaki watu waliofika hapo ingawa mvua ikinyesha.

Ijumaa, 3 Aprili 2015

Garissa:Maandamano dhidi ya Alshabab

Maandamano Garissa

Wananchi wa mji wa Garissa nchini Kenya wamefanya maandamano kupinga vitendo vya kundi la Al Shabaab, lililoshambulia chuo kimoja kikuu mjini humo na kuwaua watu 147 wengi wao wakiwa wanafunzi hapo jana.

Waandamanaji pia wameelezea kutoridhika na vyombo vya usalama nchini humo wakisema havikuchukua hatua za kutosha kutoa ulinzi kwa waliouawa na kwa raia wengine kwa jumla.

Wazazi, jamaa na marafiki wa wanafunzi waliouawa katika chuo kikuu cha Garissa wamekuwa wakiendelea kuwasili katika eneo hilo kuitambua miili ya wapendwa wao.

Waliojeruhiwa wanaendelea kupata matibabu .

Garissa

Serikali ya Kenya imekuwa ikiwasafirisha manusura wa shambulio hilo kwa mabasi kuelekea makwao huku miili ya waliouawa ikisafirishwa mjini Nairobi.

Wakati huo huo rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema Somalia na Kenya zinafaa kuimarisha uhusiano wao katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Tamko hilo linajiri siku moja baada ya shambulio hilo la Alshaabab katika chuo kimoja kikuu mjini Garrisa

Lady jaydee na Atemi waachia ngoma mpya

Msanii wa Kenya, Atemi na mwanamuziki wa Tanzania Lady Jaydee wametoa kibao kipya kwa jina 'MOYO'.

'Moyo' ni wimbo kuhusu mapenzi ya matukio tofauti .

Katika wimbo huu Atemi anasema kuwa haijalishi penzi lina mvuto wa kiasi gani mwishowe bado linasalia kuwa penzi.

Wimbo huo uliotungwa na Atemi Oyungu ni 'single' ya kwanza kutoka album yake mpya ya tatu.

Wimbo huo umeandaliwa na R-kay ambaye pia aliandaa wimbo mwengine wa Atemi 'Usijali' akiimba na Delvin Savara wa Sauti Sol.


Huyu ndio mshukiwa mkuu wa shambukizi la chuo kikuu cha Garisa nchini Kenya

Amri ya kutotoka nje yatolewa Garisa

Serikali ya Kenya imetangaza amri ya kutotoka nje usiku kwa muda wa wiki mbili katika kaunti kadhaa kaskazini mashariki mwa Kenya.

Amri hiyo iliyotolewa na mkuu wa polisi nchini humo, imetolewa baada ya wanamgambo wa kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia kuwaua zaidi ya watu 147.

Mbunge wa eneo hilo, ambaye pia ni kinara mkuu wa upande wa wanasiasa wengi bungeni, Aden Bare Duale, ameiambia BBC kuwa Waziri wa maswala ya ndani ya taifa anafanya mkutano wa dharura wa usalama mjini Garissa.

Serikali imetoa zawadi nono kwa mtu atakayetoa ripoti ya kukamatwa kwa mhusika mkuu katika shambulio hilo.

Amri ya kutotoka nje yatolewa Garisa

Serikali ya Kenya imetangaza amri ya kutotoka nje usiku kwa muda wa wiki mbili katika kaunti kadhaa kaskazini mashariki mwa Kenya.

Amri hiyo iliyotolewa na mkuu wa polisi nchini humo, imetolewa baada ya wanamgambo wa kundi la Al shabaab lenye makao yake nchini Somalia kuwaua zaidi ya watu 147.

Mbunge wa eneo hilo, ambaye pia ni kinara mkuu wa upande wa wanasiasa wengi bungeni, Aden Bare Duale, ameiambia BBC kuwa Waziri wa maswala ya ndani ya taifa anafanya mkutano wa dharura wa usalama mjini Garissa.

Serikali imetoa zawadi nono kwa mtu atakayetoa ripoti ya kukamatwa kwa mhusika mkuu katika shambulio hilo.

Jumatano, 1 Aprili 2015

Yousou ndour ndie Mwanamuziki tajiri Africa

Usanii wa muziki ni miongoni mwa kazi zinazolipa vizuri duniani.

Hatahivyo si kila mtu anayefanikiwa katika sekta ya muziki.

Kulingana na mtandao wa capital Fm nchini Kenya,kwa wewe kufanikiwa ni sharti uipende sekta hii pamoja na uwajue wateja wako.

Hivyo ndivyo wasanii wengi wa muziki wameweza kujitengezea jina duniani.

Na je, unawajua wanamuziki tajiri barani Afrika?Orodha ya wanamuziki 10 walio matajiri barani afrika kulingana na Answers Afrika itakushangaza.

Hii Hapa.

01.Youssou N'Dour - Senegal.

02.P-Square- Nigeria

03.D'banj - Nigerian

04.Koffi Olomide - DRC

05.Salif Keita - Mali

06.Fally Ipupa DRC

07.Face Idibia - Nigeria

08.Hugh Masekela - South Africa

09.Banky W - Nigeria

10.Jose Chameleon - Uganda