Jumanne, 17 Machi 2015

Arsenal yalala kwa monaco yashindwa kusonga ulaya

Pamoja na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
wakiwa ugenini katika mchezo uliopigwa usiku wa
kuamkia leo, washika bunduki wa jiji la London
Arsenal wameshindwa kusonga mbele katika hatua
ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa
barani Ulaya kwa kosa la kuruhusu magoli mengi
wakiwa nyumbani katika mchezo wa awali,
ambapo Monaco iliwabamiza wenyeji wao hao
Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1.
Arsenal ilijipatia goli la kwanza dakika ya 36
ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Olivier
Giroud kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la
pili katika dakika ya 79 ya mchezo huo.
Matokeo ya jumla kwa timu hizo ni 3-3 japo
Monaco inasonga mbele kwa faida ya kuwa na
magoli mengi ya ugenini na kuwaacha vijana
wa mzee Wenga wakikosa kufika robo fainali
kwa mara ya tano mfululizo. Kitimtimu hicho
cha klabu bingwa Ulaya kilitimua vumbi pia
huko nchini Hispania pale, Atletico Madrid
ilipowakaribisha Bayer Leverkusen kutoka
Ujerumani. Katika mchezo huo wenyeji
Atletico wamefanikiwa kusonga mbele kwa
mikwaju ya Penati baada kumaliza dakika 120
wakiwa mbele kwa bao moja ambalo
halikutosha kuamua mshindi kutokana na
matokeo ya mchezo wa awali ambapo
Leverkusen iliibanjua Atletico bao moja kwa
bila. Wakiwa mbele ya mashabiki wao lukuki
Atletico ilishinda penati 3 dhidi ya 2 za
wageni wao na kutinga moja kwa moja katika
hatua ya robo fainali wakiungana na ndugu
zao Real Madri. Ligi hiyo itaendelea tena leo
hii kwa michezo miwili kupigwa. Borussia
Dortmund watavaana na Juventus huku miamba
ya soka ya Hispania Barcelona ikiialika
Manchester City kutoka England.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni