Chama cha Likud cha Waziri Mkuu Benjamin
Netanyahu kimepata ushindi wa kushangaza katika
uchaguzi mkuu wa Israel. Vimeripoti vyombo vya
habari vya Israel.
Matokeo ya awali yalionyesha chama cha
mrengo wa kushoto cha Zionist Union kupata
mshitiko.
Huku kura nyingi zikiwa zimehesabiwa, Likud
kinaonekana kupata viti 29 katika bunge lenye
viti 120, huku chama cha Zionist Union
kikiwa na viti 24.
Matokeo haya yakithibitishwa, itaonyesha
kuwepo kwa serikali nyingine ya mseto
itakayoongozwa na Bwana Netanyahu.
Yitzhak Herzog kiongozi wa chama cha
mrengo wa kushoto cha Zionist Union
Bwana Netanyahu atahitaji kuungwa mkono
kutoka vyama vingine ili kuunda serikali ya
mseto.
Katika hotuba kwa wafuasi wake mjini Tel
Aviv baada ya kufungwa kwa vituo vya
kupigia kura Jumanne, Bwana Netanyahu
amesema tayari amezungumza na viongozi wa
vyama vingine vyenye mrengo wa kulia kuhusu
kuunda serikali mpya "bila kuchelewa".
Bwana Netanyahu amehodhi siasa za Israel
kwa muda mrefu katika kipindi cha miaka 20.
Kiongozi wa muungano wa vyama vya mrengo
wa kushoto wa Zionist Union Yitzhak Herzog
amekishutumu chama tawala cha Likud kwa
kudidimiza viwango vya maisha ya raia wa
Israel na amekuwa akipiga kampeni dhidi ya
sera za nje za Bwana Netanyahu.
Jumatano, 18 Machi 2015
Chama cha Likud chashinda uchaguzi Israel
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni