Jumamosi, 8 Februari 2014

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LANUKIA

 
sauti za busara

SABUNI ZA KURUDISHA UBIKIRA NI BALAA


Sabuni za kurudisha ubikira balaa'

WANAWAKE wameshauriwa kuacha kutumia sabuni za kunawia sehemu za siri ambazo hudaiwa kurejesha ubikira kwani zina madhara makubwa ikiwemo kusababisha kansa ya shingo ya kizazi. Mkaguzi wa Dawa na Mfamasi...a wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi wakati wa uteketezaji dawa, vipodozi na vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu....
Photo: ‘Sabuni za kurudisha ubikira balaa'

WANAWAKE wameshauriwa kuacha kutumia sabuni za kunawia sehemu za siri ambazo hudaiwa kurejesha ubikira kwani zina madhara makubwa ikiwemo kusababisha kansa ya shingo ya kizazi. Mkaguzi wa Dawa na Mfamasia wa Manispaa ya Dodoma Daria Mwanuka alisema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi wakati wa uteketezaji dawa, vipodozi na vyakula visivyofaa kwa matumizi ya binadamu.... Soma zaidi http://tinyurl.com/mmuydkx

Ijumaa, 7 Februari 2014

JE WAJUA KUHUSU VALENTINES DAY SOMA HAPA.....

Siku ya wapendanao au Valentine's day ina historia ndefu sana. Swahilivibe tunawaletea historia ya siku hiyo kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya historia ya siku hiyo.

Asili ya siku ya wapendanao "Valentine's Day" ni St Valentine, mhubiri wa kikristo aliyekuwa akiishi karibu na mji wa Roma katika karne ya tatu wakati wa utawala wa Claudis II.

Claudis alitaka awe na jeshi kubwa akategemea vijana wangejitolea na kujiunga na jeshi lake.

Lakini vijana wengi hawakupenda vita kwakuwa hawakutaka kuziacha familia zao na watoto wao.

Claudis akafikiria akaona hawa vijana kuwakomesha waingie jeshini ni kupiga marufuku watu kuoana.Kuanzia hapo akapiga marufuku watu kuoana akitegemea vijana hawatajali sasa kujiunga na jeshi kwasababu ya familia zao.

Askofu Valentine naye kwa siri akawa anawafungisha ndoa vijana hao kwa siri.

Claudius aliposikia habari hizo aliamuru Valentine akamatwe na akahukumiwa adhabu ya kifo cha kunyongwa.

Wakati akiwa jela akisubiri siku yake ya kunyongwa Valentine alikuwa akitembelewa na vijana waliokuwa wakimpelekea maua kuonyesha wako pamoja nae.

Mmoja wa vijana waliokuwa wakienda kumtembelea ni mtoto wa mkuu wa gereza ambaye aliruhusiwa kuingia mpaka kwenye selo la Valentine "kupiga naye stori".

Inasemekana kwamba Valentine aliangukia katika mapenzi na binti huyo wa mkuu wa gereza wakati anasubiria kunyongwa.

Inasemekana kwamba muda mchache kabla hajanyongwa Valentine aliomba kalamu na karatasi na kuandika meseji yake ya kuaga akiweka sahihi "From Your Valentine" ( kutoka kwa Valentine wako )

Valentine akanyongwa tarehe 14 februari mwaka 269 AD.

Baada ya kunyongwa kwa Valentine, vijana wa Roma walianza kumuiga Valentine na kuwaandikia na kuwatumia wanawake waliowapenda salamu za mapenzi.

Tangia siku hiyo tarehe hiyo ikaanza kuhusishwa urafiki, upendo na mahaba duniani huku ikihusishwa zaidi na mambo ya mapenzi.

Siku hiyo imezidi kuwa maarufu kila miaka inavyoenda huku huku makampuni yakiigeuza siku hiyo kuwa ya biashara zaidi kwa kufanya kila kitu maalumu kwa siku ya wapendanao kionekane kuwa inabidi kiwe chekundu kuanzia kadi za salamu, maua, mpaka nguo wavaazo wapendanao inabidi ziwe nyekundu.

Kuna watu wengi pia ambao hawasherehekei siku hii kwa kuhoji umuhimu wa kuonyesha kumjali umpendaye katika siku moja tu ya mwaka badala ya siku zote 365.

kama unasherehekea siku hii
HAPPY VALENTINE'S DAY FROM

RAISI WA TFF AFIKISHA SIKU 100 ZA UONGOZI WAKE

Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Gamal Malinzi amesema siku miamoja za uongozi wake katika shirikisho hilo amekutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja kukuta madeni mengi pamoja na mikataba isiyokuwa na tija.
Photo: Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Gamal Malinzi amesema siku miamoja za uongozi wake katika  shirikisho hilo amekutana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja kukuta madeni mengi pamoja na mikataba isiyokuwa na tija.

IKULU YATAJA MAJINA 201 YA WATAKAINGIA KWENYE BUNGE LA KATIBA

Ikulu imetaja majina ya wajumbe 201 watakaoingia kwenye bunge la katiba ambapo kati ya wajumbe 201 wajumbe 21 ni wazee kuanzia miaka 65.

Baadhi ya majina yaliyoingia ni Prof. Ibrahim Lipumba, prof. Abdalah Safari , Paul kimiti, Kingunge Ngombale Mwiru, Peter Kuga mziray, Christoper Mtikila, John Lifa Chipaka, Emmanuel Makaidi ,Godfrey Simbeye, Kajubi Mukajaga, Paul Makonda na Julius Itatiro.
Aki...tangaza majina hayo kwa niaba ya rais kaimu katibu mkuu kiongozi Dr. Florence Turuka amesema wajumbe walitakiwa 201 ingawa majina yaliyopendekezwa yalikuwa 3,936.

Wajumbe hao wataungana na wabunge wa bunge la jamhuri na wawakilishi kutoka baraza la Zanzibar katika kujadili rasimu ya pili ya katiba na kuifanyika marekebisho kabla ya kuingia hatua ya kura ya maoni.
Mvua iliyoambatana na upepo mkali uliovuma usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam umesababisha umeme kukatika kwa zaidi ya saa sita katika sehemu kubwa ya jiji hilo,miti kuanguka pamoja na wavuvi kusitisha shughuli za uvuvi ili kunusuru maisha yao huku mamlaka ya hali ya hewa ikisema upepo kama huo huenda ukaendelea kutokea nchini hadi Jumatano ijayo.

Swahili vibe imepita katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam majira ya asubuhi na kushuhudia miti ikiwa imeanguka pembezoni  mwa barabara pamoja na nguzo za umeme zikiwa katika hali ya kutaka kudondoka .
Katika sehemu kubwa ya jiji la Dar es Salaam umeme ulikatika wakati upepo huo ukivuma  ambapo  mafundi wa  shirika la umeme Tanzania -Tanesco wameonekana  majira hayo ya asubuhi wakiwa katika harakati za kurejesha umeme.