Jumanne, 28 Aprili 2015

Jeshi la Nigeria lawaokoa wasichana 293

Jeshi nchini Nigeria

Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.

Jeshi limeiambia BBC kwamba wanawake na watoto hao wa kike walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao baada ya kuziharibu kambi hizo.

"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."

Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok.

"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote

Jumamosi, 25 Aprili 2015

Choko choko za wenger na morinho zaanza

Arsene Wenger

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemjibu mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger baada ya Wenger kuhoji kuhusu mbinu inayotumiwa na Chelsea kulinda lango lake.

Wenger alimchokoza kocha huyo wa Chelsea akisema kuwa ni rahisi kulinda lango,swala lililomshinikiza Mourinho kumjibu akisema kuwa iwapo kulinda lango ni rahisi ni kwa nini Arsenal walibanduliwa katika michuano ya kufuzu kwa robo fainali walipolazwa 3-1 na Monaco.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ya ligi ya Uingereza itakayochezwa katika uwanja wa Emirates siku ya jumapili.

Alhamisi, 23 Aprili 2015

Basi laua 10 shinyanga

Habari  zilizotufikia  zinaarifu  kuwa  basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.

Watu 10 wamefariki na  50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.





Jumatano, 22 Aprili 2015

Mama Lulu afunguka mazito kuhusu mwanawe

Kufuatia kuandamwa na skendo za wanaume na kuchafuliwa kila siku, mama mzazi wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’, Lucresia Karugila ‘Mama Lulu’ ametoa kauli nzito yenye kushtua kwamba anatamani mwanaye huyo afe tu ili watu wanyamaze kumsemasema. Imemuuma sana!

Mama Lulu amefunguka hayo siku kadhaa baada ya mitandao ya kijamii kuchafuka kwa habari za binti yake na wanaume hasa wa watu huku mwenyewe (Lulu) akiwa nyumbani kwake Mbezi-Beach jijini Dar akiwa hana hili wala lile.

Akizungumza na gazeti la Risasi, mama Lulu alisema mambo mazito kuwa, hakuna mzazi ambaye hata siku moja anaweza kuvumilia kuona mtoto wake akiandamwa na kashfa ambazo si za kweli.

“Mimi ndiye nimemzaa Lulu, najua uchungu wa mtoto kama mzazi.
“Wanaomsema Lulu vibaya wakumbuke hata mimi nina moyo kama wao, si chuma hivyo hata mimi naumia kama ambavyo mwanamke yeyote mwenye kujua uchungu wa mwana ni nini anaweza kuumia.“Ni mzazi gani mwenye moyo wa chuma wa kuona mwanaye anabebeshwa shutuma nzito kama hizo kila kukicha halafu akanyamaza au kufurahia?

“Watu wanamfuatilia na kumsakama sana mwanangu. Hawamwachi apumue,” alisema mama Lulu kwa uchungu huku machozi yakimtoka.

Jumanne, 21 Aprili 2015

Hukumu ya morsi kusomwa leo

Mohamed Morsi

Mahakama nchini Misri inatarajiwa kutoa hukumu kwenye kesi kadha zinazomkabili rais wa zamani Mohammed Morsi ambaye aliondolewa madarakani na jeshi mwaka 2013.

Anakabuliwa na kesi pamoja na viangozi wengine wa kundi la Muslim Brotherhood kwa kuwachochea wafuasi kumuua mwandishi wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya rais mwaka 2012.

Mawakili wanamtetea bwana Mosri wamasema kuwa huenda akakabiliwa na hukumu ya kifo. Mamia ya wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood wamehukumiwa kifo katika mikakati ya kukabiliana na kundi hilo lililopiwa marufuku na rais wa sasa Abdul Fattah al-Sisi.

Kundi la Muslim Brotherhood limemlaumu rais kwa kutumia mahakama kama silaha

Ethiopia yaanza cku 3 za maombolezo

Islamic State wakienda kuwaua raia wa Ethiopia

Ethiopia imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kwa heshima za raia wake waliouawa na wanamgambo wa kundi la Islamic State nchini Libya.

Bendera zitapepea nusu mlingoti wakati nalo bunge la nchi hiyo likikutana kujadili hatua ambazo litachukua kufuatia mauaji hayo ya raia wake zaidi ya ishirini.

Msemaji wa serikali Redwan Hussein, alisema kuwa waathiriwa hao wanaaminika kuwa wahamiaji waliojaribu kusafiri kwenda barani ulaya.

Mungano wa Afrika ambao una makao yake makuu nchini Ethiopia ulilaani mauaji hayo na kusema kuwa utafanya mikakati ya kuhakikisha kuwepo usalama nchini Libya.

Wanamgambo wa Islamic State walitoa kanda ya video ambayo inakisiwa kuonyesha mauaji hayo yanayoonyesha watu hao wakipigwa risasi na kukatwa vichwa.

Jumatatu, 20 Aprili 2015

Wahamiaji 20 zaidi wazama bahari ya mediterania

 Wahamiaji waliokolewa Mediterenian Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo la IOM watu ishirini wameripotiwa kufariki. Aliyetoa ujumbe huo wa dharura amesema, boti tatu zinahitaji misaada katika eneo la kimataifa la bahari hiyo. Mawaziri wa muungano wa Ulaya, EU, wanakutano mjini Luxembourg, leo kujadili mzozo huo wa uhamiaji baada ya mamia ya watu kuzama mwishoni mwa juma lililopita, baada ya boti yao kuzama katika pwani ya Libya. Afisa mkuu anayehusika na masuala ya nchi za kigeni wa EU, Federica Mogherini, amesema kuwa mataifa ya bara Ulaya yanapaswa kushughulikia tatizo hilo la wahamiaji katika bahari ya Mediterranean. "Tunawajibika kisiasa na kwa misingi ya kibinadam kutekeleza majukumu yetu. Bahari ya mediterenian ni letu na ni sharti tuchukuE hatua kama raia wa Ulaya. Ni kwa manufaa yetu, hadhi ya muungano wa ulaya na dhamira kuu ya kuundwa kwa muunganoi huu ni kulinda haki za kibinadam, heshima ya binadamu na masiha ya watu, ni lazima tuzingatie hayo'' Alisema Mogherini. Baadhi ya mataifa ya Kusini mwa Ulaya yanasema kuwa hadhi ya EU, imehujumiwa kufuatia uamuzi wake wa mwaka uliopita wa kupunguza shughuli za uokozi. Umoja wa Mataifa umesema njia ya kutoka Kaskazini mwa Afrika hadi Italia na Malta imegeuka na kuwa hatari zaidi duniani.