Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City
watamuuza Yaya Toure msimu huu katika mpango
unaolenga kuwauza wachezaji wengine wa kilabu
hiyo kwa lengo la kununua wachezaji chipukizi
watakaoongozwa na mchezaji Kevin De Bruyn wa
Wolfsburg.
Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona
katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya
kombe la vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha
kwamba mabadiliko makubwa yanahitajika
katika kilabu hiyo.
Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa
katika mechi dhidi ya Barcelona ni Sergio
Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini
ya umri wa miaka 27.
Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet
Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa
na maisha marefu katika kilabu hiyo
,waliosalia huenda wakauzwa.
Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary
Sagna,Martin Demichelis,Alkesandar Kolarov
,Samir Nasri na James Milner ambaye
kandarasi yake inaisha hatma yao haijulikani.
Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa
katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumatano
usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus
Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin
Dzeko huenda pia wakauzwa.
Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili
kujiunga na kilabu ya New York City nchini
Marekani.
Alhamisi, 19 Machi 2015
Mancity kumtema yaya toure
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni