Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne S. Makinda
(Mb),
anasikitika kutoa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe. Saidi Ramadhani
Bwanamdogo Kilichotokea
leo (Jumatano) asubuhi tarehe 22.1.2014 Katika hospitali ya
Muhimbili/MOI alikokuwa amelazwa kwa Matibabu.
Mipango ya Mazishi zinaendela kufanywa na Ofisi
ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu, ambapo mazishi yanatarajiwa
kufanyika kesho siku ya Alhamisi tarehe 23 Januari, 2014 kijijini kwake MIONO, Wilaya ya BAGAMOYO, Mkoa wa PWANI. Taarifa zaidi juu ya msiba
huu zitaendelea kutolewa na Ofisis ya Bunge
kadrizitakapopatikana.
“Inna llilah Waina
Illaih Rajiun!”
Imetolewa na
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusianao wa
Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
DAR ES SALAAM
22.01.2014.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni